USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Thursday, January 31, 2019

Mambo ya msingi ya kuzingatia ili kuepukana na ugonjwa ya figo

Ili uweze kujikinga na janga litokanali na ugonjwa wa figo basi unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:

Usichelewe kwenda kujisaidia haja ndogo. 
Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo baya. Kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu. Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu huzidisha bakteria haraka.

Mara mkojo unaporudi nyuma ya njia na Figo, sumu dutu husababisha maambukizi ya figo, pia njia ya mkojo na "nephritis", pamoja na "uremia". Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya hivyo haraka iwezekanavyo.

Usile Chumvi kupita kiasi. 
Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku.

Usile nyama kupita kiasi. 
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng'enyo wa Protini unazalisha amonia- sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako. Nyama nyingi inaleta uharibifu zaidi wa figo.

Usinywe "Caffeins" kwa wingi. 
Caffein hutokana na vinywaji vya Soda na vinywaji vingine laini kama Kahawa, Redblue n.k. Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza mateso. Unapaswa kupunguza kiwango cha Coke, Pepsi, Red Bull, nk ambavyo hunywa kila siku.

Kunywa maji. 
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri. Endapo hatunywi MAJI ya kutosha, sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu, kama hakuna kimiminika cha kutosha kutoa kwa njia ya figo. Unashauriwa  Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku.

Kuna njia rahisi ya kuangalia kama unakunywa maji ya kutosha: Angalia rangi ya mkojo wako; Wepesi wa rangi, ndiyo vizuri.


Share:

Tuesday, January 22, 2019

Njia za kuepukana na madeni

Hakuna mtu anayependa kuwa na madeni, lakini mara nyingi watu hujikuta katika madeni makubwa. Kwa kiasi kikubwa watu wengi huingia kwenye madeni kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha matumizi kuliko kipato.

Madeni siyo kitu kizuri hasa ikiwa hayatalipwa kwa wakati. Swala la kuepuka madeni ni swala linalohitaji maamuzi sahihi ya kifikra pamoja na mikakati stahiki.

Je unapenda kuepuka au kupunguza kiwango chako cha madeni? Karibu nikufahamishe njia  za kuepuka madeni.

1. Jiwekee bajeti binafsi
Utawasikia watu wakikosoa bajeti ya serekali lakini hawana bajeti zao binafsi. Bajeti binafsi ni muhimu kwani hukuwezesha kupanga juu ya mapato na matumizi yako.

Ili kuepuka madeni, ni muhimu kuweka bajeti binafsi ambayo itakuongoza juu ya matumizi yako ya pesa ili usije ukatumia kuliko kipato chako.

2. Epuka matumizi yasiyo ya lazima
Kuna matumizi chungu nzima ya pesa, lakini matumizi ya lazima ni machache. Ikiwa kipato chako ni kidogo hakuna haja ya kufanya mambo kama vile kununua simu au nguo za gharama kubwa.

Nimeshuhudia baadhi ya watu wakikopa mikopo kwa ajili ya sherehe na matumizi mengine ya anasa. Mambo kama haya huwaingiza watu wengi kwenye madeni makubwa, hivyo yakupasa kuyaepuka.

3. Epuka kukopa bila mpango
Watu wengi hushindwa kurejesha mikopo kutokana na kukopa bila mpango. Inatakiwa kabla ya kukopa uhakikishe una mpango mzuri unaoonyesha jinsi utakavyotumia na kurejesha mkopo huo.

Kumbuka pesa ya mkopo hasa kutoka kwenye taasisi za kifedha inatakiwa irejeshwe kwa wakati tena kwa riba. Hivyo epuka kutumia pesa za mkopo bila mpango unaoeleweka vyema.

4. Epuka ushawishi wa marafiki kwenye matumizi
Watu wengi hutumbukia kwenye matumizi makubwa au yasiyo na ulazima kutokana na ushawishi wa marafiki kwenye matumizi yao ya pesa.

Hakikisha kila unachokinunua au kutumia pesa yako kina maana kwako na hakitakupotezea pesa zako. Kumbuka mrejeshaji wa mkopo ni wewe na wala siyo rafiki yako


5. Tumia kidogo kuliko unachopata
Mara nyingi matumizi huwa makubwa kuliko kipato; na hii ndiyo sababu kubwa ya watu kukopa pesa. Hakikisha unajitahidi kutumia pesa kidogo kuliko zile unazozipata ili ujiwekee akiba na uweze kukidhi mahitaji yako ya msingi.

6. Weka akiba
Kuna kipindi cha shibe na njaa kwenye uchumi; hivyo unahitaji kujiandaa kwa vipindi vyote. Mara nyingi watu hukopa pindi wawapo na uhitaji.

Kwa njia ya kujiwekea akiba utaweza kuwa na pesa hata wakati huna kipato. Kumbuka! Kuweka akiba siyo kuwa na pesa nyingi bali ni maamuzi tu.

Kwa hakika nidhamu ya matumizi ya pesa ni jambo muhimu sana katika kuepuka madeni. Naamini pia kama utazingatia hoja jadiliwa hapo juu huku ukihakikisha unakuwa na matumizi mazuri ya pesa, utaweza kupunguza kama siyo kuepuka madeni maishani mwako.
Share:

Hizi ndio faida za vazi la Kanga kwenye ndoa

Katika kuifanya ndoa iwe imara, niliwahi kuzungumzia mavazi sahihi ya mke kumvalia mumewe wakiwa chumbani. Lakini pia nikasema kwamba, kama kwenye nyumba mnaishi wawili tu, sioni shida mke kuvaa anavyotaka.

Pia nikasema kuwa, hakuna kitu kibaya kama mke wa mtu kuvaa nguo zisizo za heshima kwenye nyumba ya kupanga kiasi cha kuwatega wapangaji wa kiume.

Nilisema hayo baada ya kubaini kuwa, wapo wanawake ambao wameolewa lakini hawaoni hatari kuvaa kimitego bila kujali kuwa, kufanya hivyo ni kuiweka rehani ndoa.

Kuna hili vazi la kanga moja ambalo baadhi ya wanawake wamekuwa wakipenda kulivaa hasa maeneo ya mjini, bila kujali ni mchana au usiku, kwenye nyumba ya kupanga au binafsi.

Hapo ndipo penye shida na leo nimeona nilizungumzie ili wale wenye tabia hiyo waache mara moja kama wanazitaka ndoa zao.

Niseme tu kwamba, ukiwa na mumeo chumbani wala sioni tatizo kumvalia kanga moja, wakubwa wanajua faida ya vazi hili katika kuidumisha ndoa.

Pia ikiwa mnaishi peke yenu, siyo hatari hata kidogo kuvaa kanga moja, akazurura nayo sebuleni, jikoni na sehemu nyingine za nyumba yenu. Nasema hivyo kwa sababu, kuvaa minguo kibao mbele ya mumeo naweza kusema ni ushamba, labda kama kuna baridi sana, unaumwa au hauko vizuri na mwenza wako. Kinyume chake unaweza kuvaa vazi hilo na ikawa ni chachu ya mambo yetu yalee.

Shida inakuja pale utakapovaa vazi hilo kisha kutoka na kwenda bafuni kuoga, mbaya zaidi uwe umejaaliwa umbile tata kisha kwenye nyumba unayoishi kuna wanaume kibao. Unadhani katika mazingira hayo ndoa yako itakuwa salama kweli?

Unadhani wapangaji wenzako watakuheshimu? Sidhani kama itakuwa hivyo. Kwa kuvaa kanga moja ni wazi utapata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume wakware na wengi watakuona unatangaza biashara. Mumeo naye hawezi kufurahia hilo, labda awe ni miongoni mwa wale malimbukeni.
Unachotakiwa kujua ni kwamba, kuvaa kanga moja hasa kwa mke wa mtu na kukatiza mbele za wanaume bila aibu ni kujichoresha. Utadharaulika na hata mumeo hawezi kupata heshima inayostahili kwani ataonekana kaoa mke mcharuko.

Labda niseme tu kwamba, unatakiwa kuwa makini sana na mavazi yako. Tambua uvaeje ukiwa na mumeo tu chumbani, uvaeje ukitoka kwenye geti la nyumba yenu na uvaeje ukiwa ndani ya nyumba huku ukiwa na familia.

Wapo wanaokosea, unakuta mke wa mtu ana watoto tena wakubwa tu lakini akiwa ndani kwake anaona sawa kuvaa kanga moja na akawa anazunguka huku na kule. Hii siyo sawa! Ni kweli wanao hawawezi kukutamani lakini unawafundisha nini kwa kuvaa hivyo?

Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, unapoingia kwenye ndoa unatakiwa kujitofautisha kabisa na wale ambao wako ‘singo’. Kanga moja ni vazi la kumvalia mumeo tena hasa chumbani.

Usijidhalilishe kuvaa nguo ambayo itakufanya utafsirike tofauti, udharaulike na kuonekana unatangaza biashara wakati una mume.
Share:

Dalili nne ambazo ukiziona kwenye mahusiano ujue mnaendana

Wataalamu wa mahusiano wanasema kuwa kuna dalili nne ambazo ukiziona kwenye mahusiano yako basi amini kuwa ninyi mnaendana na pia mapenzi yenu yatadumu

1. Uhusiano wenu uwe na uwiano.

Mahusiano ambayo yamefanikiwa ni yale yenye uwiano sahihi. Katika mahusiano mtakuwa tofauti wakati mwingine, na utofauti huu lazima ulete ulingano.

Mfano, kuna ambao hupenda sana kutoka out na marafiki, huyu anahitaji kupata mtu ambaye si mpenzi sana wa kwenda out ili kuleta mlingano. Unatakiwa kuwa na mtu ambaye unakamilika unapokuwa nae, mtu ambaye mkiwa pamoja mkichanganya tabia zenu mnapata tabia moja ambayo imetokana na kuathiriana kwa matendo yenu.

2. Mnafurahia kusafiri pamoja.

Njia rahisi kabisa ya kujua kama mnaendeana ni kama manafurahia mnapokuwa manasafiri pamoja, Watu wanaoendana hupenda kusafiri pamoja na kwenda sehemu tofauti tofauti.

 Kama wewe unataka kusafiri kwa gari, lakini mwenzako anataka kupanda ndege na ubishani wenu unakuwa mkubwa basi ujue ninyi manatatizo. Wapenzi wanaoendana hukubaliana na njia moja ya kutumia ambayo wote wataifurahia.

3. Uliyenaye anakufanya ujisikie vizuri.

Kuwa katika mahusiano ambayo yanakufa ujisikie kuwa upo katika ubora wako, sio mahusiano ambayo kila ukiyakumbuka unanuna.Kuwa na uhusiano na mtu ambaye mkikaa pamoja huhitaji kupiga miayo na kujinyoosha ili upate cha kuongea. Kuwa na mahusiano ambayo yanakufanya uone fahara hata kuyazungumzia mbele ya rafiki zako.

4. Kuna kitu mnachokipenda ambacho mnafurahia kukifanya pamoja.

Hii ni muhimu kuiona, watu wanaopendana huwa kuna kitu kimoja au zaidi ambavyo wote mnapenda na hufurahia kukifanya pamoja. Hii haimaanishi kuwa basi vitu vyenu kama ni muziki, au vitu vingine vitakuwa sawa, lakini kuna kitu ambacho kitakuwa kinaingiliana kati yenu na ambacho mnafurahia kukifanya.

Kwa ufupi mtakuwa na labda vitu viwili au vitatu mnavyopenda kufanya pamoja mfano kuogelea, kuangalia tamthiliya, muziki, kutembea na vingine. Hii ni ishara kuwa ninyi
Share:

Mwanaume ambaye hakutaki umtajua kwa tabia hizi hapa

Kuna ishara nyingi ambazo ni vyema tukajifunza ili kuwa makini na kuchukua hatua pale unapoziona kwa mwanaume. Ni vigumu kukubaliana nazo lakini ukweli siku zote huwa unabaki palepale lazima tujifunze kama ifuatavyo:

Kutokujali

Ukiona mwanaume ameacha kabisa kukujali. Tofauti na namna ambavyo alikuwa mwanzo kwamba atakuuliza umekula, upo wapi ujue kabisa mtu huyo ameshakutoa moyoni. Kwa mtu unayempenda haiwezekani vitu hivyo vikakata ghafla na vikadumu kwa muda mrefu.

Mwanaume anakaa wiki moja, mbili na hata mwezi mzima bila kukuuliza chochote, jiongeze na uanze kuchukua hatua za kumtoa moyoni. Kama mtu hakujali ni dhahiri hana mpango na wewe, utateseka bure kuendelea kumuwaza wakati yeye anafurahia maisha ya uhusiano na mtu mwingine.

Mwanaume alikuwa akikupigia simu kila wakati, akikutumia ujumbe kila wakati lakini ghafla ameacha na anakaa muda wa mwezi au miezi bila kukupigia wala kukutumia uijumbe wowote, huyo hakutaki. Yeye hawasiliani na wewe lakini wewe kila uchwao ndiyo unakazana kumpigia.

Mbaya zaidi hata simu zako hapokei, hilo ni tatizo. Si mara moja au mara mbili unafanya hivyo lakini hajali, tambua kabisa unapoteza muda wako bure.  Mwanaume huyo anakuwa tayari ana mtu mwingine au alichokuwa anakitafuta kwako ameshakipata au pengine matarajio yake kwako sivyo alivyotegemea.

Mwingine anakuwa mtu wa kukuita pale tu anapokuwa na matamanio ya kimwili. Anakuita na baada ya hapo, hazungumzi na wewe tena. Hakupi ushirikiano wowote hadi pale atakapokuwa anahitaji kuonana na wewe ndipo anakupigia simu kwa kujifanya anakusalimia ili ukimjibu vizuri, anaomba muonane faragha.
Share:

RSS BAND SONG; MWAMINI MUNGU (NEW OFFICIAL)

Share:

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL