USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Sunday, October 21, 2018

Ajali mbaya yatokea Singida, Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anapenda kuwataarifu ya kuwa Wizara ya Kilimo imepatwa na msiba wa Watumishi wake Watano (5) waliopata ajali leo asubuhi tarehe 21 Oktoba, 2018 Manyoni mkoani Singida, walipokuwa safarini kuelekea Mwanza kikazi. Watumishi hao waliofariki ni;
1. Stella Joram Ossano (39)
2. Esta Tadayo Mutatembwa (36)
3. Abdallah Selemani Mushumbusi (53)
4. Charles Josephat Somi
5. Erasto Mhina (43)

Miili ya marehemu ipo njiani kuja Hospitali ya Mkoa wa Dodoma leo tarehe 21 Oktoba 2018.

Mungu azilaze roho zao mahala pema peponi, Amina🙏🏿
Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha kwenye ajali ya gari iliyotokea eneo la Njirii wilayani Manyoni mkoani Singida leo Oktoba 21.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, kamishna msaidizi wa polisi Sweetbert Njewike, amesema kuwa ajali hiyo imehusisha magari mawili ikiwemo gari dogo mali ya Wizara ya Kilimo na Chakula iliyokuwa na watu watano pamoja na lori.

Kamanda Njewile amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari ndogo iliyokuwa katika mwendokasi ikijaribu kupishana na lori.
"Gari ndogo mali ya Wizara ya Kilimo na Chakula ilikuwa ikitokea Dodoma kwenda Shinyanga ikiwa na watumishi wa wizara hiyo, ilikuwa katika mwendokasi na kugongana uso uso na Lori", amesema Kamanda Njewile.

Kamanda amewataja waliofariki kuwa ni wanawake wawili na wanaume watatu na wote wamehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Manyoni.
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL