USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Friday, October 26, 2018

CCM: "Uchaguzi 2020 atashinda mmoja tu CHADEMA"

Baadhi ya wabunge wa CHADEMA wakiwa kwenye maandamano

Mbunge wa jimbo la Siha Mkoani Kilimanjaro kupitia CCM, Dkt Godwin Mollel amesema hajutii uamuzi wa kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa kile alichokidai amefanikiwa kutatua baadhi ya kero ambazo zilikuwa zinamkabili ndani ya jimbo lake.

Mbunge huyo ambaye alikuwa ni miongoni mwa wabunge wa mwanzoni ambao walitangaza kuihama  (CHADEMA), ambapo licha ya kuwepo kwa upinzani, mkali alifanikiwa kutetea jimbo hilo.

Akizungumza na www.eatv.tv Dkt Godwin Mollel amesema “wanaosema nimepotea ni kwamba mimi naishi jimboni kwangu, tofauti yangu na wao mimi sina kiherehere, ukienda Siha asilimia 81 ya barabara ya lami imekamilika, zimeshaingia milioni 600 kwa ajili ya hospitali ya wilaya, sasa hivi nahangaikia bilioni 1.7 kwa ajili ya maendeleo”.

“Sitakaa nijutie kuhama CHADEMA, ndio maana nimeungwa mkono na niliwaambia watu huwa siingii vita ya kitoto, na sijaingia vita ya kitoto, pia nimesikia wataondoka wabunge karibia wote na watabaki kumi, na wakati wa uchaguzi atashinda mbunge mmoja ambaye kwa sasa siwezi kumtaja”, ameongeza Dkt Godwin Mollel.

Desemba 14 mwaka jana Godwin Mollel alitangaza kujivua uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kuhamia CCM ambayo ilimfanya apoteze nafasi yake ya ubunge wa jimbo la Siha
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL