USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Wednesday, October 17, 2018

Jinsi ya Kumuingiza mwanamke kwenye Mahusiano nawe na Akupende.

Hakuna mwanamke anayeamka kitandani asubuhi na kuomba... "Mungu, natumaini leo utanisaidia nisikongwe moyo na mwanaume yoyote".

Rafiki yangu mmoja amekuja kunitembelea leo kwenye makao makuu , akiwa na swali ambalo linalenga na linafaa kuwa katika kolamu ya waulize wanaume, jamaa alikuwa analaani sana kuwa amechoka sana kuishi maisha ya peke yake, maisha ya upweke. 

Alikuwa anasema hivi na sio kuwa wasichana hawapo mitaani, anachomaanisha anasema hao waliopo siku hizi kila mtu na mtu wake, kila anae mfuatilia anakutana na kufuri, alishafungwa na mwanaume mwingine, hawana hisia na yeye na anashindwa kuelewa tatizo hasa ni nini na inakuwaje hapo, hili jambo limenishitua akilini na nikajiuliza na kuhisi labda kuna wengine wengi kama yeye wanaohitaji msaada wa kutatuliwa hili jambo hivyo ikanibidi msaada wake niubadilishe uwe mada ili tuelimishane hapa kiumeni.com

Tutengeneze mfano wa jambo kwa uhalisia, umemfukuzia huyu msichana, mwisho wa siku anakupa jibu kavu, kwa sababu zote zilizopo, anakuambia "Ooh, huu kidogo sio mda mzuri wa mie kuwa na mpenzi" au anakuambia kitu kama "Sasa hivi nahitaji muda kidogo niweke mambo yangu sawa", au anakuambia lile jibu nalolipenda sana "Kwa sasa nipo bize sana na kazi yangu, sina muda wa kitu kama hicho", hivi kwa akili yako kabisa unaweza amini hizo sababu ambazo amekupa?, nahisi hata yeye mwenyewe haamini hizo sababu alizokupatia, unajua kwanini?

Kwasababu anakudanganya, sio ya kwamba kwa sasa hivi ni mda mbaya wa wewe na yeye kuwa wapenzi, na sio ya kwamba anahitaji nafasi, na zaidi ya hapo hata kama kazi zake za kiofisi zinambana, haziwezi kuwa zinambana kihivyo anavyojielezea, anachokimaanisha hapo ni "Nipishe, ondoka karibu yangu" au inawezekana anasema "Kajipange upya na kataarishe vizuri hizo swaga zako ndo uje we mjinga".

Kwa tafiti za kisayansi na kihisabati, na kama wewe ni msomaji halisi wa kiumeni.com utakuwa unalijua hili. Asilimia 60% ya maongezi ya kibinadamu huwa ni ishara, ambazo huwa tunaziita lugha za mwili. Asilimia 30% huwa ni sauti zisizo na maana na hivyo ndivyo ilivyo, hivyo ukiunganisha hapo kwa hesabu za kibongo tunajikuta asilimia 90% ya mawasiliano ni vitu ambavyo hujavipangilia kuvizungumza kupitia kwenye mdomo wako.

Hio inajulikana lazima huyo msichana akudanganye, ni mtu mwema sidhani kama anataka akuumize hisia zako, ungetaka akuambie nini maana hata kukujua bado hajakujua.

Kwa bahati nzuri tunalijua jambo moja hapa kiumeni.com kwa ufasaha na uelewa wa hali ya juu, kama tulivyo sie wengine, wanawake wazuri huwa hawajui ni nini wanachokihitaji mpaka wakione mbele yao kwa macho, unachotakiwa sasa ni kumfungua macho yake na kumuonyesha jinsi ulivyo wewe, akuone upande wako wa kibinadamu ufurahishao, upande ambao utamfanya azimike na wewe, upande ambao unafurahisha mtu akiwa nawe karibu.

Haijalishi ni kipi, haijalishi ni wapi, haijarishi ni nani. Mwanaume yeyote anauwezo wa kumkonga moyo mwanamke yeyote yule, ila anachoitaji ni mbinu sahihi za kufanya hivyo na hio ndo kanuni kuu.

Mwanamke anauwezo mkubwa wa kutambua uhalisia, anauwezo wa kugundua iwapo unajifanyisha na hicho umwambiacho ni cha uwongo au ukweli kwa kukusikiliza tu. Hii hutokana na uzoefu wa wao katika utongozwaji, hivyo wanaume wengi hujikuta wakikataliwa kutokana na kutokuwa na uhalisia na kile wanachokiongea na zaidi ya hapo kutokuwa na kujiamini kwa yale wanayoyatamka.

Huwezi kutumia kile ambacho hauna, kwa hio usiigize kuwa unacho maana hakitakupa msaada wowote, kama wewe ni mtu mwenye kuona aibu, kuwa na aibu ila itumie katika hali itakayokunufaisha wewe, na kama wewe ni mtu wa mitoko ya hapa na pale. Tumia hicho kipaji ulichonacho cha mitoko. Inawezekana hajaitaji kusikia ukweli wote kuhusu wewe ila jua anahita akufahamu, na inawezekana haitaji kuona yote kuhusu wewe kwa mkupuo ila jua angependelea kuyaona.

Tumia kujiamini, msome na mjue jinsi gani alivyo na nini anachopendelea na mwache naye akuelewe wewe, ila hakikisha hautoi maelezo yote kuhusu wewe kwa mkupuo maana hio itamfanya awe amekuelewa na atakosa kile cha kujiuliza juu yako, kile kitu akilini ambacho angependa kujua zaidi kuhusu wewe, utakua umeua ila hisia ya hamasa ya kupenda kukufahamu zaidi, mwache akuelewe kidogo kidogo, mwache akufunue kama kitabu, karatasi moja baada ya nyingine na utamu utamzidia wa kukutaka kukujua zaidi na utafanya hisia zake ziamke na hamasa yake ya kukufahamu wewe iwe kubwa zaidi.

Muombe mtoke pamoja, na kuna kiwango kikubwa inawezekana akakubali, na atakapokubali kutoka nawe, hata kama hajaonesha wazi kuwa ampendezwa nawe, kumbuka saa zote jionyeshe kwa uhalisia, uhalisia wa kuwa wewe kama wewe.

Pale utakapokuwa unajiuliza nini cha kumwambia au ni jinsi gani muonekano wako ulivyo au iwapo kama kweli amependezewa na wewe, kumbuka ameshakubali kutoka nawe katika mtoko!, na hio inamaanisha amepangua ratiba zake na kuweka ratiba ya kutoka mtoko nawe wakati alikuwa na uwezo mkubwa tu wa kukataa, na hivyo inamaanisha sio tena kazi yako ya kujaribu kumfanya apendezwe na wewe, ila ni kazi yako kumfanya afurahie kuwa na wewe na zaidi ya hapo umfanye  afurahie kila sekunde ya yeye kuwa na wewe.

Hizi ndizo kanuni za kiumeni.com, ukiwa unaongea naye msikilize, weka akili yako yote kuelewa yale anayoyaongelea na mjibu kama inavyopaswa, mwanamke huwa anaingiwa na akshi ya kuzungumza iwapo yule anayeongea nae anamjibu na kuonyesha yupo kwenye hayo maongezi wanayoyaongelea kwa asilimia 100%, kwa hio usiwaze mengine au kuhamisha macho yako na kuanza kumwangalia matiti au midomo yake kwa jinsi aongeavyo, huko kutamfanya apate hisia haupo kwa ajili ya kumpenda yeye ila lako ni jambo moja tu, kile kilicho katikati ya miguu yake, macho yako yanatakiwa yawe yamegongana na yakwake ila yasiwe katika hali ya kuzua maswali.

Kugonganisha macho na mwanamke kunaleta taswila ya kujiamini, na zaidi ya hapo huleta hali ya huba na mahaba, msikilize na mjibu. Ili ikifika muda wako wa kuongea utapata yakuongea kulingana na yale aliyokuwa akiyaongelea, muulize maswali kuhusu yeye, kuhusu mambo anayopendelea. Wanawake hupenda kujiongelea na utaonekana unajali hivyo kumuongezea mvuto juu yako.

Kutokea hapo kitachofuatia ni mtoko wa pili, na itakuwa mtililiko wa mapenzi baada ya hapo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL