MFANYABIASHARA MOHAMED DEWJI.
Lugola aliyasema hayo jana alipokua akijibu maswali ya waandishi wa habari katika ziara yake ya kushtukiza katika Kituo cha Kati cha Polisi Dodoma.
Alisema Jeshi la Polisi linaendelea na kazi yake kama ilivyokawaida kwa kuwasaka watuhumiwa wote ambao wameshiriki katika matukio yote ya kiahalifu likiwamo la kumteka Dewji.
“Kila siku pamekuwa na maneno mbalimbali katika maeneo mengi nchini, watu wanahoji walimteka Mo kana kwamba watu wengi waliofanyiwa uhalifu kama huo, wao hawaapaswi kufuatiliwa na Jeshi la Polisi…sisi tunaendelea na kazi zetu kama ilivyo kawaida na sio kuwatafuta waliomteka ‘Mo’ tu bali hata wale katika matukio mengine,” alisema Lugola.
Alisema anasikitishwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipiga kelele katika vyombo mbalimbali vya habari kulishutumu Jeshi la Polisi na kuliingilia katika utendaji wake wa kazi.
“Hawa ambao wanapiga kelele leo kuwa waliomteka ‘Mo’ watakamatwa lini ndiyo ambao walipiga kelele kuwa Jeshi la Polisi haliwezi kuwapata na kutaka vyombo vya nje ya nchi yetu, lakini kutokana na umakini wa jeshi letu lilifanikiwa kubana njia zote za watekaji,” alisema.
Aidha aliwataka wananchi kubadilika kwa kuacha tabia za kukuza mambo na kuonekana kuwa baadhi ya watu ndiyo wenye haki na wale maskini hawastahili kupewa kipaumbele na Jeshi la Polisi.
Awali akizungumzi juu ya ziara yake hiyo ya kushtukiza alisema lengo lake ni kukagua maagizo yake anayoyatoa nchi nzima kama yanatekelezwa.
Alisema katika ziara hiyo amebaini kuwa bado upo upungufu ambao haujafanyiwa kazi na kuwataka wakuu wa polisi wa mikoa yote nchini kuyatekeleza kabla hawajaondolewa katika nafasi za
0 comments:
Post a Comment