Moja kati ya taarifa zilizotufikia leo October 28 2018 ni pamoja na stori ya helicopter ya Bilionea na mmiliki wa club ya Leicester City Vichai Srivaddhnapprabah kuanguka na kuwaka moto.
Helicopter hiyo imeanguka na kuwaka moto sekunde chache baada ya kupaa kutoka katika uwanja wa soka wa King Power ambao ndio uwanja wa nyumbani wa club ya Leicester City
Kwa mujibu wa mashuhuda waliyoshuhudia ajali hiyo wameiambia Sky Sports kuwa kabla kuanguka helicopter hiyo ilitoa mlio usiokuwa wa kawaida kuashiria kuwa chombo hiko kibovu
Makamu mwenyekiti club ya Leicester City ya England Aiyawatt Srivaddhanaprabha na mkurugenzi wa club Jon Rudkin hawakuwepo kwenye helicopter hiyo wakati inapata ajali
0 comments:
Post a Comment