RC Makonda ameandika haya:
Siku ya leo nimetimiza miaka saba ya ndoa yangu, lakini nikitizama njia tuliyopita bado nawaza tumewezaje kufika na ndipo ninapomrudishia MUNGU utukufu.
Pamoja na uhai tuliopatiwa, naamini MTOTO ni moja ya zawadi kubwa ambayo wanandoa huitegemea na kumlilia MUNGU usiku na mchana waipate, leo ninayo furaha kubwa kusherehekea nikiwa na mtoto wa kiume anaejulikana kwa jina la KEAGAN, Namshukuru MUNGU kwasababu haikuwa rahisi, na najua kuna wengine ambao wamekata tamaa ndani ya mwaka 1, 2, na wengine hata ndoa zao kuvunjika kwasababu ya kutokupata mtoto, lakini JAWABU LA MUNGU hutoka kwa wakati wake.
Naendelea kumshukuru sana MUNGU kwa kunipa mke aliepita nami katika mabonde na milima, hata pale Dunia iliponiacha MARIA WANGU hakuthubutu hata kwa sura kuonesha hayuko pamoja na mimi, Ilifika wakati narudi kazini nikiwa naweweseka lakini alionesha tabasamu na kuniambia MUNGU YUPO, alinifuta machozi usiku wa manane nilipopaza sauti na kumlilia MUNGU tena akiwa pembeni tukiomba pamoja, pale ninapoamka asubuhi na kukuta magazeti yamechafuka na kuandika kila aina ya habari bado mke wangu alisema NAMUAMINI MUNGU HATA HILI ATAKUVUSHA, na hata mitandao ya kijamii ikinisema kwa kila namna na wengine kwenda mbali zaidi na kutoa kila aina ya tusi, bado mke wangu aliendelea kuniamini, kuniombea na kunishika mkono, alifanyika kuwa kila unachokijua kuhakikisha kwamba sikati tamaa, na kwa hilo sina zaidi ya shukurani za kipekee kwake, nafahamu umri wangu wa ndoa sio mrefu kuliko wengine ambao wako katika ndoa miaka 10, 20, lakini kwa yale niliyoyapitia inatosha kusema ASANTE MUNGU KWA KUNIPA MKE MWEMA.
Kipenzi changu Maria, wewe ni amani yangu, pepo yangu, pumzi yangu na mboni ya macho yangu, Hutetereki, Huyumbishwi na wala humuangalii yeyote mwingine isipokuwa MIMI, naachaje kukushukuru MUNGU wangu kwa Baraka hii kubwa!! Siku ya leo naahidi kuikumbatia, kuilinda na kuienzi milele mpaka kifo kitakapotutenganisha.
Zaidi ya yote nimshukuru MUNGU kwa kuniongezea KAMANDA mwingine kwenye familia, maana nilizoea kuisikia sauti yako tu ikinifariji, lakini naamini kuna sauti nyingine imeongezeka itakayokuwa ikiniambia "DADDY, YOU CAN DO IT"
Asante MUNGU kwa kunifanya niitwe BABA!!!
0 comments:
Post a Comment