USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Sunday, October 21, 2018


STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford amesema kuwa, anashangaa kila akiposti chochote mtandaoni watu wanasema ameachika, jambo ambalo halina ukweli na wanaosubiri aachike, watasubiri sana.

Shamsa alisema kila akiweka ‘status’ kwenye ukurasa wake wa Instagram inayohusu ishu za kuachana, kuna wanaodhani inamhusu yeye, wakati huwa kuna ambao wamekuwa wakiomba ushauri na kwa sababu hawezi kumshauri kila mtu kwa wakati wake, huamua kuandika kwenye ukurasa wake. “Unajua nilipoweka ‘status’ kila mtu alinihoji na wengine kunifuata ‘DM’ wakitaka kujua nini kimenikuta, niwaambie tu kwamba sitaachika mpaka Mungu atakapotutenganisha ingawa wapo wanaoniombea hilo kila siku,” alisema Shamsa.

Shamsa alitupia ‘status’ inayosomeka hivi: ‘Mapenzi au kumpenda mtu, kusikufanye uwe mtumwa… ukiona unampenda mtu halafu anakuchukulia poa achana naye. Maisha ya sasa hivi, siyo ya kujipendekeza au kulazimishana… mtu uwaze maisha magumu bado mapenzi yakusumbue? Acha ujinga na usikubali kuwa mtumwa… wewe funika sura fanya kama huoni..


Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL