Hapa duniani kuna mapenzi ya aina mbili(selfish love and unselfish love)mapenzi ya uchoyo na mapenzi yasio ya uchoyo,mapenzi ya uchoyo ni yale mapenzi ambayo mpendwa mmoja wapo hupenda kupendwa yeye tu kujaliwa yeyetu, pasipo kurudisha upendo kwa mwenzie vile inavyotakiwa kwa lugha nyingine mtu mwenye mapenzi ya uchoyo huwa sio mbunifu katika kupendezesha penzi na mara nyingi huwa ni mtu mwenye lawama na ambae haridhiki kwa kila jambo zuri atakalofanyiwa,(unselfish love)mapenzi yasiyokuwa ya uchoyo haya ndio mapenzi ya kweli,watu wenye mapenzi ya kweli huwa wanapenda kutoa kuliko kupewa na pia hutoa pasipo kuwa na matarajio ya kupata kitu flani.
Bali kutoa kwao ndio furaha ya moyo wao,kama ni mwananke anakuwa anamjali sana mpenzi wake pale anapokuwa na vijisenti kidogo akiona shati ama suruali nzuri ambayo anahisi mpenzi wake itampendeza lazima amnunulie,wakati mwengine humsaidia mpenzi wake pesa pale anapohisi mpenzi wake hana kitu nia yake nikutaka mpenzi wake awe na furaha mda wote na pia mwanamke huyu huwa hapendi kupokea pesa ya mpenzi wake pale anapopewa labda awe na shida kubwa sana.
Ukweli kabisa mwanamke yoyote akimpenda mwanaume humfanyia yote hayo mwanaume,ukiona mwanamke anajifanya anakupenda na hakufanyii hayo,ujue huyo hakupendi yupo kimaslahi tu, labda awe mwanamke wa hali ya chini sana,na kwa upande wa mwanaume akimpenda mwanamke kweli,huwa anajali sana ikiwa pamoja na kutoa huduma kulingana na uwezo wake,humshirikisha mpenzi wake kwenye mipango yake na kama ni hatua za uchumba huwa hana haraka sana ya kula papuchi kwasababu anajua nimali yake anakuwa na subira tu,kwa lugha rahisi naweza nikasema humjali sana mpenzi wake hasa kwenye huduma zote zinahusiana na maswala ya kifedha kwasababu anajua ni wajibu wake.
Note:kwenye mapenzi ya kweli hata hao wanawake wanaojiita(Gold digger),huwapatia pesa wanaume zao,hata wanaume wanaojifanya wabahili huwa wanatoa pesa nyingi tu kwa wanawake wa wapendao.
0 comments:
Post a Comment