MAOMBI: KUFUNGA NA KUOMBA KWA AJILI YA MACHO YA ROHO NGUVU YA MUNGU NDANI YETU
“Na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; KWA KADIRI YA UTENDAJI WA NGUVU ZA UWEZA WAKE” #WAEFESO 1:19
Nakusalimu mwana wa Mungu katika jina la Yesu Kristo aliye hai.
Namshukuru Mungu mwenye neema ambaye ameendelea kusimama pamoja nasi katika maombi yetu haya tangu ijumaa. Nikutakie ibada njema wewe ambaye leo ni siku yako njema ya kuabudu.
Namshukuru Mungu mwenye neema ambaye ameendelea kusimama pamoja nasi katika maombi yetu haya tangu ijumaa. Nikutakie ibada njema wewe ambaye leo ni siku yako njema ya kuabudu.
Tumeendelea kumwona Mungu akiwasaidia watoto wake kwa namna ya ajabu sana kwenye maombi haya. Wale ambao walikuwa hawawezi kufunga Roho wa Kristo amewatia nguvu na wamejikuta wakiweza. Unajua tunapomwamini Mungu yeye hufanya vitu kwa jinsi ya tofauti sana. Lakini pia namtolea Mungu shukrani kwa wote ambao wamekuwa wakimpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao kwenye maombi haya. Na wale ambao wamekuwa wakitengeneza mahusiano yao na Bwana Yesu.
Kwa wale ambao yamkini walichelewa kujua taarifa za maombi haya usikate tamaa. Wiki ijayo tena tutakuwa na maombi kama haya kuanzia Ijumaa hadi jumapili. Na usiache kutuombea kwa ajili ya huduma ambayo kuanzia wiki kesho tutakuwa nayo kijiji cha Bukumbi wilaya ya Uyui mkoani tabora. Tuombee Mungu atufunike na uweza wake. Usikose maombi ya wiki ijayo. Leo pamoja na maombi yako binafsi uliyonayo nataka uungane nasi tuombe kwa ajili ya kuomba kuwa na nguvu ya Mungu ndani yako.
Kwa wale ambao yamkini walichelewa kujua taarifa za maombi haya usikate tamaa. Wiki ijayo tena tutakuwa na maombi kama haya kuanzia Ijumaa hadi jumapili. Na usiache kutuombea kwa ajili ya huduma ambayo kuanzia wiki kesho tutakuwa nayo kijiji cha Bukumbi wilaya ya Uyui mkoani tabora. Tuombee Mungu atufunike na uweza wake. Usikose maombi ya wiki ijayo. Leo pamoja na maombi yako binafsi uliyonayo nataka uungane nasi tuombe kwa ajili ya kuomba kuwa na nguvu ya Mungu ndani yako.
Mpendwa Mungu hutupa nguvu tunazozihitaji kwa ajili ya kufanikiwa katika maisha. Hutupa nguvu za kufanikiwa kwenye Nyanja mbalimbali za maisha yetu kama tukidhamiria kumtumaini. Yeye anasema ‘Utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake’ #KUMBUKUMBU 8:18. Kumbe hata fedha na mali na utajiri tulio nao ni Mungu ametupa nguvu ya kuvipata. Hatuna hata sababu ya kuvilingia hata tushindwe kumtolea yeye kidogo kwa ajili ya kazi yake.
Huwa tunasikia kuhusu nguvu na uweza wa Mungu ambao umekuwa ukitenda mambo mbalimbali kwenye maisha ya watu mbalimbali kwenye historia ya Biblia. Nguvu ya Mungu iliyokuwa ndani yao na juu yao. Hata leo bado iko nguvu ya Mungu itendao kazi ndani ya watakatifu wake ambao wamedhamiria kumtegemea Mungu. Nguvu hiyo na uweza huo unatusaidia dhidi ya mambo mbalimbali. Tunajua uweza na nguvu ya Mungu inayoweza kutusaidia tunapokuwa tumeshambuliwa na nguvu za Shetani kwenye biashara zetu, kwenye ndoa zetu, tunapopoteza kazi, wakati afya zetu zinapotetereka, tunapokuwa kwenye maumivu makubwa moyoni ya kutalikiwa au kukataliwa na wanawake au wanaume, au kutelekezwa na wenzi wetu, tunapokuwa kwenye mazingira ambapo ndoto zetu zinakuwa kama zimeyeyuka kwa sababu ya mazingira fulani fulani. Swali la msingi ambalo tunaweza kujihoji ni je namna gani tunaweza kutegemea nguvu hiyo ya Mungu?
Majibu yanajificha kwenye msingi wa mstari wetu unaobeba somo letu la leo. Nguvu hii ya Mungu ndani yetu hufanya kazi ndani yetu kwa IMANI. Kama wafuasi wa Kristo, tumaini letu ni kubwa kuliko tunavyojua kwa kuwa Kristo anaishi ndani yetu kwa hilo yanayotokea yeye aweza kuyashughulikia kama tutamtegemea yeye kwa imani. Mimi na wewe tunaomtegemea na kumwamini Bwana Yesu iko nguvu ya Mungu inayokaa ndani yetu. Na yamkini unajua hilo ila labda hujajijua tu kwamba Roho wa Kristo aliyemo ndani yako huaachilia nguvu ya Mungu ndani yako. Kwa nguvu hiyo tunaweza kuamuru mambo na yakatokea. Sasa inahitaji pia ujitambue kwamba iko nguvu ya Mungu ndani yako. Haijalishi ni kwa namna gani tuko kwenye shida lakini Mungu aweza kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, KWA KADIRI YA NGUVU ITENDAYO KAZI NDANI YETU #WAEFESO 3:20. Mungu hafungwi na kile tunachomuomba tu bali huenda mbali zaidi ya kile tunachomuomba au tunachokidhania.
Ninatamani kila mfuasi wa Kristo kuwa na uzoefu wa nguvu za Mungu. Kwanza awe na shauku ya kuwa na nguvu ya Mungu itendayo kazi ndani yake. “Mtakeni Bwana na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote” #ZABURI 105:4. Na maandiko yanatuasa kuwa na uzoefu wa nguvu za Mungu zitendazo kazi ndani yetu. “MZIDI kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake” #WAEFESO 6:10. Tunahitaji kuwa na uzoefu na nguvu ya Mungu ndani yetu kila siku. Ndio maana hili limekuwa ni ombi ambalo siachi kuomba maishani mwangu. Nami nikutie wivu mwana wa Mungu usiache kuomba kujazwa na nguvu za Mungu ndani yako. Tunahitaji kuwa na uzoefu wa utendaji kazi wa nguvu za Mungu ndani yetu. “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho” #WAEFESO 5:18
Mwana wa Mungu tunahitaji kuwa na uzoefu na nguvu za Mungu ndani yetu tumdhihirishe huyo Mungu tunayemtumikia. Mungu wetu si Mungu wa nadharia (theory). Mungu wa hivyo mie simtaki. Na nakutia wivu tutie bidii kumwamini Mungu na kuutafuta uso wake ili kudhihirisha nguvu ya Mungu duniani. Yanini kuwa na Mungu ambaye hatuoni nguvu zake ndani yetu na juu yetu? Umesahau imeandikwa ‘Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu’ #1KOR 4:20. Tamani na hitaji nguvu ya Mungu ndani yako mpendwa. Hili liwe ombi lako endelevu maishani mwako.
Ubarikiwe sana.
KUNA NENO GANI LILILO GUMU LA KUMSHINDA BWANA? #MWANZO18:14
Share ujumbe huu kwa wengine kama umependezwa nao ili na wao wabarikiwe.
KUNA NENO GANI LILILO GUMU LA KUMSHINDA BWANA? #MWANZO18:14
Share ujumbe huu kwa wengine kama umependezwa nao ili na wao wabarikiwe.
Kwa maombezi, unataka kupokea uponyaji au kufunguliwa kwenye kifungo chochote kile, ushauri au unatamani ujitoe kikamilifu kumtumikia Mungu na UNATAKA KUMPOKEA BWANA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO NA AKUSAMEHE DHAMBI ABADILISHE MAISHA YAKO NA TABIA MBAYA ZILIZOKUSHINDA basi wasiliana nasi kwa msaada wa Roho Mtakatifu tukusaidie 0758 443 873 AU 0712 204 937
MPENDWA WANGU UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA. UNASUBIRI NINI KUMRUDIA BWANA YESU NA KUMTUMIKIA?
0 comments:
Post a Comment