Mahusiano na afya kwa hakika vinashabiana kwani vinategemeana kwa kufanya kuwepo furaha angalau kidogo kwa mwanadamu ni wazi kama hauna mahusiano ya aina yeyote ni dhahiri afya yako itadhorota hivyo tarajia afya njema kama unamahusiano.Mahusiano ni neno pana kulingana na uzito na ugumu wa kuzingatia katika mahusiano na pia yapo mahusiano ya aina mbalimbali kama kati ya wazazi na watoto wao,familia moja na nyingine,mtu na mtu na hata shirika na shirika lakini leo nitazungumzia mahusiano ya mtu na mtu
Ni rahisi kujenga mahusiano na mtu yeyote lakini ni vigumu kudumisha na kufurahia mahusiano hayo kutokana na utofauti kama wa rika,hali ya kimaisha,tabia,imani na mengineyo mengi hivyo ni vizuri kabla ya kuanzisha mahusiano ni lazima ukubali kuzingatia vitu Fulani ili kuhakikisha unapokuwa na mahusiano yanadumu kwa wakati wote.Katika maisha tunayoishi tunategemea mahusiano ili kutoa na kupokea vitu Fulani ambavyo inawezekana vinafaida au havina faida kwa wakati mwingine vinadhoofu miili yetu
Mojawapo ya ishara ya afya njema ni furaha japo kwa wakati mwingine mtu anaweza kuwa na furaha ya usoni na wala si moyoni
JINSI YAKUTENGENEZA FURAHA YA KWELI
-Kuikubali imani yako[dini]kuwa na imani ambayo itakuongoza kutekeleza mema
-kula lishe bora[balance diet]
-Fanya vitu unavyofurahia[hoby kama kuogelea,kucheza,kuimba n.k
-Kuwa zaidi ya usafi[nadhifu na wakupendeza]
-Jikubali kabla ya mwingine kuonyesha kukubali[usitamani kuwa na maumbile ambayo ni wazi hutoweza kuwa nayo kama ufupi,urefu n.k]
-Kubali kusamehe wengine
-Fanya shughuli zako za kimaisha kwa bidii[ikiwa ni kazini,shule na hata nyumbani]
-Jisikie kuwajali,kuwapenda,kuwathamini na hata kuwasaidia wengine
Ni dhahiri furaha ya kweli haihitaji ubinafsi ni lazima kuwepo sababu ya mwingine kuongeza furaha yako japo kama kwa mazingira Fulani inawezekana kutokuwepo mtu wa kuongeza furaha yako kwa kuona hivyo unawajibu wa kuzingatia zaidi niliyoyazungumzia hapo juu ili kuhakikisha unaendelea kuwa na afya njema
Mahusiano ya mtu na mtu inawezekana yakawa ya mwanaume na mwanamke[msichana na mvulana na hata jinsia moja]
Japo watu wengi hawajali na wala kuumizwa na mahusiano ya jinsia moja na hii ni kwasababu mahusiano ya jinsia tofauti yanalenga uhitaji zaidi kwa kutoa na kupokea kitu zaidi ya kawaida,neno kawaida ni hali ya mazoea na mtu wa aina yeyote wala uzingatiaji wa kitu chochote hauhitajiki
Kama upo uhusiano wa jinsia tofauti ni wazi kipo kitu zaidi ya kawaida na ni lazima vipo vitu vya kuzingatia ili isije ikawa ni kawaida.Mahusiano yanahitaji vitu vitatu[3]pekee
-Akili
-Moyo
-Mwili
Na kwa hakika vinatakiwa kulingana na wala siyo kingine kuzidi kwa mwenzake kwani kwa kuzingatia hivyo tunaweza kuhifadhi furaha ya kweli,Akili ni uwezo wa kufikiri na kupambanua jambo na moyo ni uhifadhi kwa yaliyo mazuri na hata mabaya lakini mwili ni ukubali wa viungo vya nje na ndani ya mwili kufanya kazi hivyo ili kuwepo kwa afya njema hutegemea utendaji mzuri wa akili,moyo na mwili na
Vyote hivyo vipo ndani maamuzi yetu kwa ruksa ya mwenyezi mungu pekee hivyo tunawajibu wa kuvitumia tunavyotaka lakini matokeo ni jibu la utumiaji mzuri au mbaya vitu hivi.jiulize ni kwanini unapokea maumivu katika mahusiano ikiwa umepewa uwezo wa kutawala vitu hivi vitatu inawezekana ni uzembe wakutozingazia ulinganifu wa vitu hivi.
Ni wazi kila mmoja anatamani kuongeza furaha kwa kuwa katika mahusiano kwa kupitia blog hii inawezekana kuamua kupata mahusiano sahihi na yatakayokidhi malengo yako
NAMNA YA KUTUMIA AKILI,MOYO NA MWILI KATIKA MAHUSIANO
-AKILI katika mahusiano inatumika katika kufikiri kwamba Yule unayetamani kuwa na mahusiano naye mnashabiana kitabia,rika,hali ya maisha na mengineyo japo mengine hayana umuhumu kwa kuzingatia makubaliano ya wanamahusiano
-Moyo ni sehemu ya mahusiano kwa kupitia mbinu mbalimbali unaweza kutambua nguvu ya hisia ulizonazo kwa unayemkusudia kuwa na mahusiano naye
-mwili pia huwakilisha na kutimiza yatakayo moyo hivyo ni lazima ukubali vitu hivi kufanya kazi pamoja bila upendeleo ili kupata kitu timamu
Mahusiano ni jambo la hiyari lakini ni muhimu ili kuendeleza na kutunza furaha ya kweli na kwa kuzingatia yote hayo ni rahisi kuepuka mahusiano ya haraka na gafla
Namalizia kwa maswali ambayo nahitaji uyajibu bila mimi kusikia
-UNGE PENDA KUONGEZA FURAHA?
-JE UNAWEZA KUISHI BILA MAHUSIANO YEYOTE?
- JE UNAWEZA KUJARIBU KULA,KULALA,KUTOZUNGUMZA NA MTU YEYOTE?
-JE UNAWEZA KUISHI MAISHA YA PEKE YAKO BILA KUTOA WALA KUPOKEA CHOCHOTE KWA MWINGINE?
- JE UNAWEZA KUISHI SEHEMU AMBAYO UNAWEZA KUPATA VITU VYOTE ISIPOKUWA KUMUONA MTU WA JINSIA YEYOTE ?
Thursday, November 15, 2018
Home »
» MAHUSIANO NA AFYAJUA NAMNA YA KUONGEZA MVUTO WA KIMAPENZI
MAHUSIANO NA AFYAJUA NAMNA YA KUONGEZA MVUTO WA KIMAPENZI
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment