USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Thursday, November 15, 2018

Makala: Mwaka mchungu na mtamu kwa Diamond

Toka mwaka 2009 hadi sasa Diamond Platnumz amekuwa akifanya vizuri kimuziki na kipindi chote hicho ameweza kushinda tuzo za ndani na za kimataifa pia. Kabati lake lina tuzo kubwa zaidi ya 10 kama Channel O Music Video Awards, HiPipo Music Awards, MTV Europe Music Awards/WORLDWIDE ACT AFRICA/INDIA, MTV Africa Music Awards, African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) na nyinginezo.

Kwa mwaka huu amefanya mengi makubwa na mazuri ingawa amekuwa na changamoto kubwa kwake.Chini nimeweka yale aliyofanikiwa na yale yalimpatia changamoto kwa huu.

1. Muziki Wake

Ni mwaka ambao Diamond Platnumz amejikuta nyimbo zake tatu zikifungiwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Diamond hakuwa msanii wa kufungiwa lakini mwaka huu upepo huo umempuliza vilivyo.

February 28, 2018 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Nyimbo hizo ni zile ambazo hazikupaswa kuchezwa kwenye vyombo vya habari.

Katika orodha hiyo zilikuwepo nyimbo mbili za Diamond ambazo ni Waka aliyomshirikisha Rick Ross, pamoja na Hallelujah ambayo amewashirikisha Morgan Heritage kutoka nchini Jamaica.

Tukija hadi November 12, 2018 wimbo 'Mwanza' wa Rayvanny alioshirikiana na Diamond ulifungiwa na Basata na kuamuriwa kutolewa Youtube kabisa, pia wasanii hao wametozwa faini ya Tsh. Milioni 9. Hivyo kufanya nyimbo zake tatu kwa mwaka huu kutupwa jela ya kimuziki.

Pia ni mwaka huu ambao kwa mara ya kwanza msanii wa kwanza ameondoka kwenye lebo yake ya WCB. Rich Mavoko ambaye alisaini kuwa chini ya lebo hiyo June 2, 2016 na wimbo wake wa kwanza kutoa ulikwenda kwa jina la Ibaki Stori.

Baada ya miaka miwili Rich Mavoko ameamua kuondoka hapo na kwenda kuanzisha lebo yake ya Bilione Kid. Kuondoka kwa Rich Mavoko kumefanya WCB kusaliwa na wasanii watano ambao ni Harmonize, Rayvanny, Mbosso, Lava Lava na Queen Darleen.

2. Mahusiano

Huu ni mwaka ambao mahusiano ya Diamond yameripotiwa zaidi kwenye vyombo vya habari, hii ni kutokana na kuachana na wazazi wenzake wawili, Zari The Bosslady na Hamisa Mobetto.

Siku ya wapendanao (Valentine’s Day) February 14, 2018 Zari The Boss Lady alitangaza rasmi kuachana na Diamond kutokana na kuchoshwa na habari za kusalitiwa ambazo husikika kila siku  katika vyombo vya habari.

"There have been multiple rumors some with evidence floating around in ALL SORTS of media in regards to Diamond’s constant cheating and sadly I have decided to end my relationship with Diamond, as my RESPECT, INTEGRITY, DIGNITY & WELL BEING cannot be compromised," taarifa ya Zari ilieleza.

Hatua hiyo ilikuja baada ya September 19, 2017 Diamond kukiri kuzaa na Mwanamitindo Hamisa Mobetto licha ya kukanusha na kufanya siri kwa kipindi kirefu.

3. Biashara 

Kwa mwaka huu kwa mara ya kwana Diamond ameweza kutimiza ndoto yake ya kumiliki vyombo vya habari (Wasafi TV & Radio) na kuwa msanii wa kwanza wa Bongo Fleva kufanya hivyo.

Hatua hiyo inatafsiriwa kama mwanzo wa wasanii kuanza kujikwamua kutoka kwenye 'siasa' zilizokuwa zikiendelea kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwa kucheza baadhi ya nyimbo za wasanii kwa upendeleo na wengine kutopewa nafasi kabisa
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL