NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE.KANYASU AWAOMBA WATUMISHI WAMPE USHIRIKIANO
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu amewaomba watumishi wa Maliasili na Utalii wampe ushirikiane ili aweze kutekeleza majukumu kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John pombe Magufuli amemuamini na kumteua ili aweze kuitumikia Wizara hiyo.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwa mara ya kwanza na Watumishi hao mara baada ya kuwasili makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dodoma
Amewaomba watumishi hao wampe ushirikiano na pale mafanikio yanapopatikana yanakuwa ni mafanikio ya wizara nzima na sio ya kiongozi pekee.
‘’Mimi ni mgeni kabisa katika Wizara hii, Nahitaji ushirikiano wenu ili niweza kutimiza majukumu yangu’’ Amesema Mhe. Kanyasu
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mhe. Kanyasu amewaonya watumishi wenye tabia ya kupika majungu kuwa kwake hawana nafasi hiyo na anachotarajia nikuona kila mtumishi anatimiza majukumu yake.
‘’Ukiniletea majungu nakusikiliza halafu nikikutana na mhusika namwambia vyote ulivyosema ’’ ameonya Mhe.Kanyasu
Awali, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Lusius Mwenda amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa Watumishi wa Wizara hiyo wapo tayari kufanya kazi nae ili kuiwezesha Wizara kufikia malengo yake.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Dkt.Idd Mfunda amemhakikishia Naibu Waziri huyo kuwa watampatia ushirikiano ili Wizara iweze kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya tano
0 comments:
Post a Comment