Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu Sugu, amebainisha matumizi ya pesa zake anazoingiza kwenye muziki amekuwa akizitumia katika kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalum ikiwemo yatima.
Sugu ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini kwa muhula wa pili, amebainisha hayo wakati akimjibu moja ya wafuasi wake kupitia akaunti yake Instagram.
Katika chapisho hilo la Joseph Mbilinyi moja ya wafuasi wake aliyesomeka kwa jina la Emmanuel Syonga aliandika “Mbeya wanahitaji huduma za jamii sio tamasha.”
Akijibu Swali hilo Mbunge huyo aliandika “toka niwe mbunge fedha ninazoingiza kupitia muziki huwa zinatumika kununua sare, na mahitaji mengine ya shule kwa watoto yatima, na wale waishio kwenye mazingira magumu Jijini Mbeya.” Aliandika Mbunge Sugu.
Sugu ni miongoni mwa wasanii wa zamani wa muziki wa Hiphop ambao baadaye waliamua kujiingiza kwenye siasa na kushinda ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Saturday, November 3, 2018
Home »
» Sugu aweka wazi matumizi yake ya pesa anazopata kwenye muziki
Sugu aweka wazi matumizi yake ya pesa anazopata kwenye muziki
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment