Mpango wa Mungu kwa mwanadamu ulikuwa ni mwema sana,ukisoma
kitabu cha mwanzo unaona jinsi ambavyo Mungu aliamwandalia mwanadamu mfumo wa
maisha mazuri katika bustani ya edeni.
Mwanzo
4:7-Kama
ukitenda vyema,hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko,inakuotea
mlangoni,nayo inakutamani wewe,walakini yapasa uishinde.Haya ni maneno aliyoyatamka Mungu
akimwambia Kaini baada ya Kaini kupeleka sadaka ya mazao ya ardhi kwa
Bwana.Mungu ametupa uhuru wa kuchagua mfumo wa maisha kila mwanadamu,hivyo kila
mwanadamu anauhuru wa kuishi atakavyo na huku akisisitiza kuwa;Mtu yoyote
atakayetenda vyema,atakuwa na kibali,hii inazihirisha kuwa kuwa Mungu mapenzi
yake ni kuona tunaishi maisha ya kumpendeza yeye siku zote,ila pia ametupa
uhuru wa kuchagua aina ya maisha na ndio maana anamwambia Kaini kama ukitenda
vyema utapata kibali.
Kaini alikuwa ana uhuru wa kuchagua,kutenda
vyema au kuendelea na mfumo wa maisha aliokuwa nao,ambao kimsingi Mungu hakuupenda na ndio
maana alimwambia kama ukitenda vyema utapata kibali.Kibuli,kuzalau,kutotii
sauti ya Mungu kulimfanya Kaini aendelee kuishi maisha ambayo mbele za Mungu ni
chukizo kukampelekea kumuua ndugu yake Habili!
Kabla ya Kaini kumua ndugu yake kwa kumpeleka
eneo ambalo ni la siri(eneo ambalo halina watu ambao wangeweza kuona tukio la
Kaini kumua ndugu yake)nimekuwa najiuliza maswali kama ifuatavyo:
1:Inawezekana Kaini alifanya majaribio mengi ya kumua ndugu
yake hata kwa njia ya sumu katika
mazingira ya nyumbani akashindwa
2:Inawezekana Kaini alitumia hata watu kuwapatia pesa ili
wamuue ndugu yake ikashindikana.
3:Inawezekana Kaini alienda hata kwa
waganga kumloga Habili ikashindikana.
Haya ni baadhi ya maswali machache nimekuwa
nikijiuliza sana,na mwisho zoezi Kaini alifanikiwa kumua ndugu yake Habili
ambae alikuwa na kibali machoni pa Bwana au kwa lugha nyingine Mungu alikuwa
anamkubali Habili kwa sababu alikuwa mtii na aliishi maisha ya kumpendeza
Mungu.
KWA NINI MUNGU ALIRUHUSU KIFO CHA HABILI
USIKOSEKUFUATILIA MTILILIKO WA SOMO
HILI KILA SIKU,
0 comments:
Post a Comment