USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Saturday, October 27, 2018

Bilioni 20 za Mo kwa Simba zapangiwa matumiz

Mohammed Dewji ambaye ni mmiliki wa asilimia 49 ya hisa za klabu ya Simba.

Mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti wa klabu ya Simba Swed Mkwabi, ameweka wazi mipango yake na kuomba wanachama wa klabu hiyo wamchague.

Kampeni za uchaguzi huo wa Simba utakaofanyika November 4, 2018, zimefunguliwa rasmi jana, na leo Mkwabi ameweka wazi mipango yake kwa kusema atahakikisha pesa ya uwekezaji bilioni 20 itakayotolewa na Mohammed Dewji inaongezeka maradufu.

''Bilioni 20 ni pesa nyingi lakini inahitaji weledi mkubwa wa kuifanya endelevu, inaweza ikachotwa ndani ya miaka mitatu ikaisha tukashindwa kuzalisha tena tukarudi tulikotoka kwa hiyo kama nitapata fursa kwa kushirikiana na wenzangu tutatengeneza misingi ya kibiashara kuitoa katika bilioni 20 kuifanya iwe zaidi'', ameeleza.

Aidha Mkwabi amesema kuwa ameshagundua wanachama wa Simba wanataka wajumbe wenye mtazamo wa kimaendeleo kwa ajili ya Simba na anaamini wanajua kuchuja mjumbe gani anafaa na yupi hafai hivyo hata akiwa mwenyekiti anajua atapata wajumbe bora
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL