USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Saturday, October 27, 2018

Zaidi ya Washiriki 30,000 wathibitishwa Rock City Marathon

Zaidi ya Washiriki 30,000 kutoka ndani na nje ya nchi wamethibitishwa kushiriki mbio za Rock City Marathon msimu wa tisa zinazotarajia kufanyika Oktoba 28, Mwaka huu ambapo zitaanzia Daraja la Furahisha na kuishia Viwanja vya Rock City Mall jijini hapa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini hapa mapema hii leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Zenno Ngowi, amesema wanatarajia kuwa na mbio zenye mafanikio makubwa mwaka huu kwani maadalizi kwa kiasi kikubwa yamekamilika ambapo bado wanaendelea na usajili wa washiriki hadi leo jioni, Oktoba, 27, Mwaka huu.

Ngowi amesema kuwa pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia Shilingi Milioni Nne, kila mmoja, shilingi milioni Mbili kwa washindi wa pili,  milioni Moja washindi wa tatu, huku washindi wa Nne hadi kumi wakiibuka na zawadi na pesa taslim na medali kila mmoja.

Kwa upande wa mbio za kilomita 21, Ngowi amesema kuwa pamoja na medali washindi wa kwanda wanaume na wanawake watajinyakulia shilingi milioni tatu kila mmoja, shilingi milioni moja kwa washindi wa pili na shilingi 750,000/- kwa washindi wa tatu huku pia washindi wa nne hadi kumi wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja.

Alibainisha kuwa mbio za kilomita tano zitahusisha watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) ambapo washindi kwa upande wa mashirika, watapatiwa zawadi za utambuzi ikiwemo medali na vyeti vya ushiriki huku pesa zikielekezwa kwa wshiriki wenye ulemavu wa ngozi.

Naye mmoja kati washiriki wa mashindano hayo kutoka mkoani Mara Grace Marko, amesema kuwa amekuja kushiriki ana uhakika wa kushinda au kuwemo kati ya washindi wa tatu, huku akisema amejipanga na kwake ni kipaji alichopewa na Mungu.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk. Philis Nyimbi wamethibitisha ushiriki wa washiriki kwenye mbio hizo, ambazo zitahusisha baadhi ya viongozi wa serikali, wabunge na washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali.

Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL