Tume ya Taifa ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemtangaza Ramadhan Hamza Chande wa chama cha mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa kiti cha ujumbe wa baraza la uwakilishi katika uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimbo la Jang’ombe.
Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi jimbo la jangombe Mwanapili khamis Mohammed alisema mshindi huyo amepata kura 6581 sawa na asilimia 90.5 ya kura zote halali zilizopigwa ambazo jumla yake ni jumla 7,274.
Msimamizi huyo aliwataja wagombea wengine wa vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi huo ni chama cha AFP aliyepata kura 58 ikiwa sawa na asilimia 0.8 huku mgombea wa ADA-TADEA akipata kura 131 sawa na asilimia 1.8.
“Mgombea wa CUF amepata kura 172 sawa na asilimia 2.4,mgombea wa DP pia amepata kura 62 ikiwa sawa asilimia 0.9 na mgombea wa SAU amepata kura 53 sawa na asilimia 0.7 pamoja na TLP amepata kura 71 sawa na asilimia 1.0”alisema Msimamizi huyo.
Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Mshindi wa uchaguzi huo aliwashukuru wananchi kwa kujitokeza kushiriki uchaguzi kwa hali amani na utulivu huku akiwaomba kuongeza ushirikiano katika utendaji wa kazi anaotarajia kuanza.
Aidha alitaja kipaumbele chake kuwa atatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2015 -2020,
Saturday, October 27, 2018
Home »
» CCM yaibuka kidedea uchaguzi jimbo la Jangombe
CCM yaibuka kidedea uchaguzi jimbo la Jangombe
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment