USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Saturday, October 27, 2018

Kocha wa zamani wa England azimia akiwa studio


Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya England Glenn Hoddle amelazimika kukimbizwa hospitali mchana wa leo Oktoba 27, 2018 baada ya kuanguka ghafla na kuzimia akiwa studio.

Glenn Hoddle ambaye ni nyota wa zamani wa Tottenham amezimia ikiwa ni siku yake yua kuzaliwa akiwa anaadhimisha miaka 61.

Tukio hilo limemkuta akiwa kazini kwenye studio za kituo kimoja cha runinga ambapo huwa anachambua michezo na kwa mujibu wa mtangazaji wa kipindi hicho, Mark Pougatch, kipindi cha leo kimeahirishwa.

Kocha huyo aliteuliwa kuwa meneja wa England mwaka 1996 na ambapo alifanikiwa kuisaidai timu hiyo kufika katika raundi ya pili ya Kombe la Dunia mwaka 1998 nchini Ufaransa.

Enzi za kucheza soka Hoddle alichezea Tottenham, Monaco na Chelsea huku timu ya taifa ya England akiichezea mechi 53. Pia amewahi kuzifundisha timu za Tottenham, Chelsea, Swindon, Southampton na Wolves.
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL