Sunday, October 21, 2018
DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya Barabara, " Tunathamini Mchango wenu
VIONGOZI wa ngazi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wamepongeza uongozi wa Kliniki ya Heameda iliyopo Bunju B ambayo imekuwa ikitoa huduma za matibabu ya moyo kwa wananchi wa wilaya hiyo na maeneo mengine huku ukiahidi kushughulikia kero ya ubovu barabara inayoelekea kwenye kliniki hiyo ambayo imetajwa kutoa mchango mkubwa kuokoa maisha ya Watanzania.
Hayo yamesemwa na ujumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni kupitia Mkuu wake wa Wilaya Daniel Chongolo na Mganga Mkuu wa halmashauri hiyo Dk.Christowell Mande wakati wa uzinduzi rasmi wa Kliniki ya Heameda ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP Reginald Mengi.
Akizungumzia Kliniki hiyo Chongolo amesema Serikali inathamini mchango wa kliniki hiyo kwa kutoa huduma kwa wananchi wa Kinondoni na hasa walioko maeneo hayo ambayo hayana vituo vingi vya afya.Pia amejibu kuhusu ombi kero ya barabara inayoingia kwenye kliniki hiyo kwa kuahidi kuishughulikia mara moja kwa kuitengeneza.
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Dk.Mande amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa sekta binafsi katika kutoa huduma za afya na iko tayari kufanya kazi na kliniki hiyo."Tunawakaribisha muda wowote kufanya kazi katika dhana ya PPP.Kikubwa ambacho tunaweza kueleza hapa ni kwamba tunathamini mchango wenu na tunaomba tuedelee kushirikiana katika kuwahudumia Watanzania,"amesema.
Wakati huo huo mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Kliniki ya Heameda Dk.Reginald Mengi amesema kijana wa Kitanzania Dk.Hery Mwandolela ambaye ndio mmikili wa Kliniki hiyo amefanya maajabu makubwa na anastahili kuwa mfano wa kuigwa
Related Posts:
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment