Sunday, October 21, 2018
Mauaji ya Mwandishi wa Habari yachukua sura mpya, Umoja wa Mataifa Waingilia kati
atibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, mashirika ya kutetea haki za binadamu na vyama vya wandishi wa habari vimetaka waliohusika na mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi nchini Uturuki waadhibiwe.
Guterres amesema amepata wasiwasi mkubwa baada ya Saudi Arabia kukiri kuwa Khashoggi alifikwa na umauti kwenye ubalozi wake mdogo.
Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa kuna haja ya kufanyika uchunguzi wa haraka na wa kina kuhusiana na kadhia hiyo ili waliohusika wachukuliwe hatua. Uturuki imeelezea kutokufurahishwa na hatua ya Saudi Arabia ya kuchelewa kukiri kwamba imehusika na mauaji ya Khashoggi na kukitaja kitendo hicho kuwa cha kufedhehesha.
Shirika la Amnesty International limesema maelezo ya Saudi Arabia kuhusu mauaji ya Khashoggi yanaonekana kufunika mauaji ya kinyama, na taarifa nyingine mbaya zinazodhihirisha kwamba Saudi Arabia inakiuka haki za binadamu. Shirika hilo la Amnesty International limeitaka nchi hiyo kuutoa mwili wa mwandishi huyo wa habari ili ufanyiwe uchuguzi kubainisha chanzo cha kifo chake.
Taarifa ya vyombo vya habari vya serikali nchini Saudi Arabia imeongeza kusema kuwa mshauri wa mahakama ya Saudi Arabia, Saud al-Qahtani na naibu Mkuu wa idara ya upelelezi Ahmed Asiri wamefukuzwa kazi.
Related Posts:
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment