Msanii maarufu wa filamu bongo, Hemed Suleiman maarufu 'Hemed phd', ameweka wazi juu ya maisha yake ya sasa kwamba ameamua kuokoka na kubadilika kitabia.
Akizungumza kwenye DADAZ ya East Africa Televisio, Hemed amesema kwamba awali alikuwa na maisha ya kupenda kubadili wanawake, lakini sasa ameamua kutulia na kuwa na mpenzi mmoja, anayetengeneza naye maisha.
Akiendelea kuweka wazi maisha ambayo alikuwa nayo mara tu baada ya kuupata umaarufu, Hemed amesema kuwa aliachana na mpenzi wake ambaye alikuwa naye tangu akiwa darasa la tatu, lakini alimuacha mara tu baada ya kurudi kwenye mashindano ya Tusker Project Fame.
“Nilipoanza umaarufu, yule demu wangu niliyeanza naye tangu darasa la tatu mpaka napata ustar alikuja tu airpot kunipokea nilipokuwa narudi kwenye Tusker Project Fame, nilijiuliza huyu kafuata nini hapa!?. Yaani niliona ashakuja kuniharibia, maana siku ile totoz zilishaniambia sirudi nyumbani, nikawa ni mtu wa watoto tu, ila kuna muda unafika unasema nakua sasa nahitaji 'future', nikaamua kutulia na mmoja sasa hivi nimeokoka kabisa, sina mambo hayo”, amesema Hemedi.
Hemedi amesema kutokana na tabia ambayo alikuwa nayo, muda mwengine hata mtu ambaye yuko naye hamuamini, lakini ameamua kumuweka wazi kwa sababu ni kweli ametulia
Thursday, October 25, 2018
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment