Wachezaji wa Taifa Stars.
Akiongea leo Oktoba 25, 2018, kwenye mkutano na wanahabari Mwakyembe amewaomba watanzania kuendelea kuchangia timu hiyo ili kambi iwe na manufaa na mwishowe timu ikaibuke na ushindi ugenini dhidi ya Lesotho.
''Uamuzi huu unalenga kuifanya Stars izoee hali ya hewa ya Lesotho ambayo ni ya baridi ili kusaidia wachezaji waingie vizuri uwanjani wakiwa hawana tatizo, japokuwa gharama ni kubwa tofauti na awali lakini tunafanya hivi kwaajili ya kufuzu AFCON'', amesema.
Mwakyembe amesema kambi hiyo ya siku 10 ya Stars nchini Afrika Kusini, pamoja na safari nzima ya kwenda Lesotho Novemba 18 inaweza kufikia gharama ya shilingi milioni 350.
Mwakyembe pia ameweka wazi kuwa serikali inashirikiana na TFF kufanya mazungumzo na mashirika ya Ndege ili kupata bei nzuri ambayo itawawezesha Watanzania wengi kusafiri ikiwemo mazungumzo na kampuni za mabasi kwa wale watakaosafiri kwa njia ya barabara.
0 comments:
Post a Comment