USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Saturday, October 27, 2018

Jambo hili ni muhimu sana katika suala la kipesa


Endapo utapata pesa na kama hatakuwa na fikra sahihi na mikakati sahihi kuhusu pesa ni lazima pesa hizo zitapotea tu.

Hivi hujawahi kuona mtu fulani alikuwa amefanikiwa sana kifedha na kwa hivi sasa mtu huyo ni maskini wa kutupwa? bila shaka umewahi kukutana na aina hii ya watu, ukweli usioujua kuhusu watu hawa ni kwamba walipata pesa lakini hawakuwa na fikra na mikakati sahihi kuhusu pesa ndio maana leo hii watu hawa wanaishi maisha ya kawaida.

Pia watu hao wamesahahu ya kwamba hakuna jambo rahisi hapa duniani kama kufirisika endapo utashindwa kutambua thamani ya pesa uliyonayo sasa.

Ukweli usiopingika ni kwamba uli uweze kubaki katika kilele cha umiliki wa fedha inahitajika nguvu ya ziada kuweza kuelewa thamani na nguvu iliyopo katika pesa.

kwani kama utashindwa kuvitambua vitu hivyo basi umaskini utaendelea kuyatawala maisha yako kila wakati.

Hivyo tambua na elewa pesa inahitaji maandalizi ya awali kabla ya kuipata, maandalizi haya ni lazima yawe ya kisaikolojia, Yaani ukipata pesa kisiwe kitu cha kushangaza bali ni kiwe kitu ambacho ulikuwa umeshajipanga kimikakati na hivyo kukupelea wewe kwenye mikakati yako ya kiutendaji moja kwa moja.

Wengi wetu tunashindwa kufanikiwa kifedha hii ni kwa sababu pesa kwetu huwa ni kama ajali, yaani mtu akizipata ndipo anapopanga afanyie nini pesa hizo, kwa kitendo hicho unazidi kujipoteza mwenyewe.

Hivyo ili uweze kumiliki uchumi wako binafsi, hususani katika suala la kipesa unatakiwa kuhakikisha ya kwamba pesa ni lazima zikutane na fikra na mikakati sahihi, kwani kama utapewa leo pesa nyingi na ukawa hauna fikra na mikakati sahihi pesa hizo hazitakusaidia kitu
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL