Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya na mshambuliaji Meddie Kageree wanatarajiwa kupata ugumu wa namba baada ya Kocha Mkuu, Patrick Aussemss kufanya mabadiliko ndani ya kikosi hicho kwa kuwahamisha Emanuel Okwi na Claytous Chama kucheza viungo wa pembeni.
Aussems amesema kuwa anataka washambuliaji wenye uwezo wa kufunga mabao na siyo kingine hivyo atatoa nafasi kwa wachezaji wenye uchu wa mabao wanapofika kwenye lango la wapinzani.
"Mimi hivi sasa nguvu na akili zangu ninazielekeza kwenye ufungaji pekee ambazo nimezianza kwenye mchezo na Alliance, nitahakikisha timu yangu inapata mabao mengi, kama mshambuliaji atakosa umakini nitamtoa.
"Ninafurahia kumuona Okwi na Chama wakifunga mabao kutoka pembeni hivyo ndivyo ninavyotaka, kama unakumbuka katika mchezo wangu na Stand United Kichuya na Kagere walishindwa kufunga, nataka wajifunze kupitia wenzao.
Kichuya hadi sasa amefunga bao moja pekee akiwa amecheza michezo nane tangu ligi kuu imeanza amefanikiwa kuanza katika kikosi cha kwanza isipokuwa katika mchezo uliopita dhidi ya Alliance alikaa benchi, huku Kagere akiwa na mabao 4
Friday, October 26, 2018
Home »
» Kagere, Kichuya watapata tabu kwa Mbelgiji
Kagere, Kichuya watapata tabu kwa Mbelgiji
Related Posts:
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment