Thursday, October 25, 2018
Martial azitosa PSG na Juventus, aamua kubaki Man United
Mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, 22, yupo tayari kuzikacha klabu za Juventus, Paris St-Germain na Bayern Munich ili asalie na Mashetani Wekundu. (ESPN).
Manchester City wapo katika harakati za kumsajili beki wa Juventus na timu ya taifa ya Brazil Alex Sandro, 27. (Sun).
Chelsea wanajiandaa kupokea £9.5 milioni iwapo Real Madrid watamteua Antonio Conte kuwa meneja wao. (Sun) Jose Mourinho anatarajiwa kupinga mashtaka dhidi yake ya kutoa lugha chafu wakati Manchester United ilipoifunga Newcastle. (Sky Sports).
Arsenal wamemuweka katika rada zao beki wa kushoto wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, 26. ( Mirror).
Jose Mourinho atamtumia mshambuliaji Romelu Lukaku Manchester United watakapovaana na Everton siku ya Jumapili. Lukaku,25, amecheza mechi nane bila kufunga goli. (Star).
Juventus wanajiandaa kupambana na Chelsea katika harakati za kumsajili kiuongo kinda Sandro Tonali,18. Kiungo huyo ananga'ara katika ligi ya Serie B na klabu ya Brescia. ( Talksport).
Mario,25, hajacheza hata mechi moja katika klabu ya Inter Milan msimu huu. (Calciomercato).
Juventus na Borussia Dortmund ni miongoni mwa klabu kubwa ambazo wanamfuatilia kiungo kinda wa Uingereza Matt O'Riley,17, anayekipiga katika klabu ya Fulham. (Evening Standard).
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment