USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Thursday, October 25, 2018

Dereva wa Dangote asakwa na Polisi

Kamanda wa Polisi Mkoani Lindi, Prudeciana Protas amethibitisha kukimbia kwa dereva wa gari aina ya lori, mali ya kampuni ya Dangote ambalo limesababisha ajali iliyopelekea vifo vya watu 5.

Kamanda huyo amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi ambapo kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo cha ajali ni gari hilo la mizigo kuacha njia yake.

Aidha kamanda huyo amesema kwa sasa jeshi hilo linaendelea kuifanyia uchunguzi miili ya waliofariki kama ilivyotaratibu za polisi kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu zao.

“tukio lilitokea saa kumi na mbili kasoro robo asubuhi, ndani ya 'hiace' ambayo ilikuwa na watu 6 ambapo watano kati yao walifariki. Chanzo cha ajali ni dereva wa roli kuhama upande wake, na baada ya kusababisha ajali dereva alikimbia na tunamtafuta, tunamuomba ajitokeze.” Amesema Kamanda Prudeciana

Katika ajali hiyo watano wamefariki na mmoja kujeruhiwa baada ya 'Hiace' yenye namba T 760 CUZ iliyokuwa ikitokea Kiranjeranje kuelekea Lindi mjini kugongwa na gari ya mizigo ya kampuni ya Dangote yenye nambari T-515 katika kijiji cha Likahakwa mkoani Lindi
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL