Alhamdulillah! Afya yangu inaendelea kuimarika, nikiwa nimeanza kazi kidogo kidogo, ninawashukuru viongozi wote wa Dini zote, wa kimila, wa Chama changu, wa Serikali, na wananchi wa Mkoa wa Tabora kwa kuamua kunitaka nirudi nyumbani kumshukuru Mungu pamoja nao. Amenipa neema kubwa sana. Alhamdulillah. Leo nafika jimboni kwetu Nzega Vijijini kuitikia wito huo kwa dua na maombi maalum. Ninawapa pole wananchi wenzangu wote kwa mshtuko mliopata pindi mlipopata taarifa za ajali ilitusibu. Mungu hakutuacha peke yetu, alitupokea kwa mkono wake wa kiume mimi na wahanga wenzangu ambao siku zetu zilikuwa bado (na hili ndiyo funzo kubwa). Pia bado mioyo na safari zetu zina majonzi ya kumkumbuka mdogo wetu Hamza Temba (PKA) aliyetangulia mbele ya haki. #HK#HumbleHK #Alhamdulillah
KAANDIKA KUPITIA UKURASA WA INSTAGRAM YAKE
0 comments:
Post a Comment