USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Saturday, October 27, 2018

Mkurugenzi NEC aridhishwa na uendeshwaji wa uchaguzi jimbo la Jangombe

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi(NEC), Dk.Athumani Kihamia alisema Tume imeridhishwa na uendeshwaji wa uchaguzi huo ambapo umekuwa wa hali ya Amani na utulivu.

Alisema asilimia kubwa ya wananchi wamejitokeza kushiriki katika kupiga kura na kwamba vituo vimefunguliwa kwa wakati kama ilivyotakiwa kwenye majira ya saa moja hivyo kiujumla uendeshwaji wa uchaguzi umekwenda vizuri.

“Watu wengi wamekuja kupiga kura kwenye vituo hivyo kwenye majira ya saa moja hadi saa 2:30 asubuhi na kila kwenye vituo vya kupiga kura hadi muda wa saa 7 walikuwa wamejitokeza katika idadi ya takribani 300 hivyo maana yake ni kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) wamejipanga vyema katika kuhamasisha wananchi katika kushiriki kwenye uchaguzi, ”alisema Mkurugenzi

Katika maelezo yake Mkurugenzi huyo aliwapongeza mawakala wa vyama vya siasa vilivyoshiriki kwenye uchaguzi huo kwa kuwa kuzingatia hali ya utulivu na kwa upande wa NEC wamejifunza namna ya uchaguzi huo mdogo ulivyoendeshwa bila ya chuki na uadui.

“Tumewauliza mawakala kama kuna changamoto zozote wamesema hakuna hivyo inaonesha ni uchaguzi wa uwazi na unaendeshwa kwenye hali ya Amani na usalama, nimeona mawakala wa vyama vyote vya siasa wamekaa mahala pamoja,wanacheka pamoja pia wagombea wa vyama vyote wanakaa pamoja  na kuzungumza hakika ni uchaguzi wa kujifunza kuwa uchaguzi si uadui na wala si vita,”alisema 

Naye Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Ramadhani Hamza Chande, alisema ameridhishwa na namna ya uendeshwaji wa uchaguzi huo na kwamba uko wazi na wa Amani.

Alisema mwitikio wa wananchi katika kujitokeza kushiriki kwenye uchaguzi huo ni mzuri watu wamejitokeza kwa wingi na kwamba amefarijika kuona uchaguzi huo ukiendeshwa kwa hali ya Amani.

“Nashukuru mungu kuona wananchi wamejitokeza kwa wingi na wanapiga kura  bila ya kuwepo kwa viashiria vyovyote vya uvunjifu wa Amani na hiyo inaonesha kuwa walizingatia vyama vyao vya siasa ambavyo viliwataka kufanya kampeni kwa hali ya Amani na utulivu na kupiga kura kwa hali hiyo,”alisema Chande

 Alisema kwa upande wake yuko tayari kupokea matokeo yeyote ambayo yatatangwaza na Tume hiyo ya uchaguzi ya ZEC na kwamba endapo akipita kwenye uchaguzi huo anatarajia kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo katika kutekeleza ilani ya uchaguzi wa CCM.

“Nitashirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo kwani maana ya uwakilishi ni kuwakilisha wananchi kwenye kuhakikisha unaweletea maendeleo ninafahamu changamoto zilizoko kwenye jimbo hili hivyo nitazitatua,”alisema Mgombea huyo

Kwa upande wake Mgombea wa ADA-TADEA, Sabri Ramadhani Mzee, alisema ameridhishwa na namna ya uendeshwaji wa uchaguzi huo hususan katika kuhakikisha unafanyika kwa hali ya Amani na utulivu.

Alisema wananchi wamejitokeza kwa wingi kwenye ushiriki wa kupiga kura kwa kutumia haki zao za kidemokrasia ya kumchagua mwakilishi wao wa jimbo hilo atakayewaletea maendeleo.

“Mimi kama mimi nitayapokea kwa mikono yote miwili matokeo ambayo yatakayotangazwa na Tume hivyo ninachowaomba wananchi kuendelea kuwa katika hali hii ya Amani na utulivu wakati tukisubiri kuhesabiwa kwa kura,”alisema Mgombea huyo

Kwa upande wake Mgombea wa CUF, Mtumwa Abdallah alisema anategemea kuibuka mshindi kwenye uchaguzi huo kwa Zaidi ya asilimia 54 na kwamba ameridhishwa na namna ya uendeshaji wa uchaguzi huo mdogo.

Hata hivyo aliwataka wanachama wa CUF kutoendelea na tabia ya kususia uchaguzi na kwamba haina faida yeyote kwa chama cha siasa kugomea kushiriki kwenye uchaguzi.

“Bado wapigaji kura wangu ni wadogo licha ya watu kuendelea kujitokeza kwa wingi na ninachotaka kuwaambia kuwa wache hivyo wajitokeze kushiriki kwenye uchaguzi tulishasema kuwa tuache tabia hiyo na ndio maana tumeshiriki kwenye uchaguzi huu mdogo,”alisema

Alisema kwa upande wake ana Imani na Tume hiyo katika uendeshaji wa uchaguzi huo na kwamba anataka kuwambia wan-CUF awali walishasusia uchaguzi sana bila ya kuwa na faida hivyo wajitokeze kushiriki kwenye kupiga kura kwenye uchaguzi huo mdogo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL