Hivi karibuni Mwekezaji Mkuu wa Simba, Mohamed Dewji 'Mo' alikumbwa na balaa la kutekwa na watu wasiojulikana alipokuwa akiingia katika Gym iliyopo Hoteli ya Collessium iliyopo jijini Dar es Salaam, aliachiwa huru baada ya siku tisa maeneo ya Gymkhana.
Jana kwa mara ya kwanza alijitokeza hadharani tangu aachiwe huru baada ya kwenda kufanya ibada ya swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Sinashiri uliopo Mtaa wa Indira Gandhi, Upanga kwa ajili ya kuwashukuru watanzania na waumini waliomuombea ili aweze kutoka salama.
Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa kikubwa alichokuwa akifanya Mo ni kuwashukuru kwani ni mahali pake pa ibada, pia alitoa sadaka ya shukurani .
"Baada ya ibada alitoa sadaka ya shukrani kwa baadhi ya watu waliokuwa msikitini hapo kisha akaondoka zake akiwa ameambatana na baadhi ya ndugu zake wa karibu," kilisema chanzo.
Kutoka kwa Mo kumechangia kwa kiasi kikubwa Simba kupata matokeo mazuri kwani mchezo wao wa kwanza waliifunga Stand United Mabao 3-0, kisha wakamfunga Alliance mabao 5-1 kesho watacheza na Ruvu Shooting.
Saturday, October 27, 2018
Home »
» Mo Dewji ajitokeza hadharani kwa mara ya kwanza
Mo Dewji ajitokeza hadharani kwa mara ya kwanza
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment