Mkazi wa Kijiji cha Isongole wilayani Ileje mkoani Songwe, Joseph Chomo (55) ameuawa kwa kupigwa na mkewe pamoja na watoto akidaiwa kuoa mke wa pili bila kuwashirikisha.
Akizungumza na Mwananchi jana, mkuu wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude alisema tukio hilo lilitokea saa sita usiku wa kuamkia jana huku akibainisha kwamba chanzo halisi kinaendelea kuchunguzwa ili kubaini ukweli.
Mkude alisema hadi jana mke na watoto wawili wa Chomo walikuwa wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi unaendelea.
Akizungumzia mkasa huo, Elifa Kalago alisema usiku huo walisikia sauti ya Chomo akiomba msaada na walipofika nyumbani kwake walimkuta amelala mlangoni huku akitokwa damu nyingi.
Alisema alipoingia ndani aliwakuta mke na watoto wawili wakisafisha damu iliyokuwa imetapakaa katika nyumba yao.
Kalago alisema baada ya kuwauliza sababu ya tukio hilo hawakutoa jibu, ndipo walipoamua kumpeleka Chomo hospitali, lakini alipoteza maisha wakiwa njiani.
Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Ikomba Kayuni alisema wanafamilia hao walikuwa na ugomvi wa siku nyingi na ulianza baada ya baba mwenye nyumba kuoa mke wa pili bila kuwashirikisha, japokuwa awali ugomvi huo ulionekana kwisha.
Hilo ni tukio la pili katika kipindi cha wiki mbili mkoani Songwe, ambapo mwishoni mwa mwezi uliopita mkazi wa Kijiji cha Bupigu wilayani Ileje alifariki dunia baada ya kupigwa na mkewe kutokana na wivu wa mapenz
Saturday, October 27, 2018
Home »
» Auawa akidaiwa kuoa mke wa pili bila kushirikisha familia
Auawa akidaiwa kuoa mke wa pili bila kushirikisha familia
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment