Gari ambalo linaaminika kutumika katika kumteka bilionea Mohammed Dewji, Mo limepatikana kando ya viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ambapo bilionea huyo aliachiwa huru.
Jana, Mkuu wa polisi Tanzania IGP Simon Sirro alisema gari hilo, Toyota Surf, liliingia Tanzania likitokea nchi jirani mnamo Septemba mosi 2018.
Sirro hakusema gari hilo lilitokea nchi gani, lakini kutokanana na namba zake za usajili AGX 404 MC, BBC ilifanya uchunguzi na kugundua ni nambari za usajili za nchi ya Msumbiji iliyopo kusini mwa Tanzania.
Hata hivyo, gari hilo hii leo limeonekana likiwa na namba za usajili wa Tanzania T 314 AXX. Bado haijafahamika namba hizo za usajili wa Tanzania ni feki ama la.
Hakuna mtu aliyekamatwa, na bado haijulikani watu waliomtelekza Mo eneo hilo walitumia usafiri gani kutoroka.
0 comments:
Post a Comment