USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Thursday, October 25, 2018

Njia za kuondoa rangi ya weusi katika mapaja na kwapa.


Njia za kuondoa rangi ya weusi katika mapaja na kwapa.

Badili mwenendo Maisha yako katika lishe na mazoezi.
Hakikisha lishe yako unapunguza wanga nzito hasa nafaka, wali nk pia punguza vyakula vyenye sukari na vionjo vya kemikali kama soda, badala yake tumia zaidi vyakula vyenye mafuta, vitamins na protini kama nyama, parachichi, samaki,nazi, mboga za majani na karanga.
Pia punguza kula gluten nyingi ambayo ni kiambata kinachopatikana kwenye  vyakula vingi vya ngano .Jitahidi kula sana matunda yenye vitamin C kwa wingi, A kwa wingi E kwa wingi, mboga za majani nk.

Majani ya Aloevera.
Chukua utomvu wa jani la Aloevera pale pale unapokata.
Paka kwenye sehemu yenye weusi na kisha acha ule utomvu kwa muda takribani nusu nasaa kisha osha na maji ya uvugu vugu/moto  Fanya hivi mara moja hadi mbili kwa siku ili kuweza kupata matokeo haraka.

Utafurahia jinsi gani mmea huu ulivyo na maajabu katika ngozi yako kwani ngozi mpya itatengezwa haraka sana na jinsi gani ilivyo mashuhuri kama strong natural antibiotics kwenye ngozi yako.

Yogurt
Kuna maajabu makubwa sana na yogurt kwani imekuwa ikitumika kama natural bleaching agent kutokana na kiini chake [ingredient] lactic asidi pamoja na zinc yenye uwezo mkubwa wa kuzuia kuharibika kwa ngozi kutokana na jasho jingi sehemu za mapaja,shingoni na kwapa.

Chukua yogurt paka sehemu husika kisha fanya massage [sugua] halafu acha kwa dk 10-15 na baada ya hapo osha na maji ya uvugu vugu.

Pia unaweza kuchukua yogurt kijiko kimoja cha chai  ukachanganya na kipande cha limao kisha paka na sugua sehemu husika rudia mara 3-4 kwa wiki.

Limao.
Limao ina uasili wa ASIDI ambao unafanya itumike kama Natural bleaching agent cha ngozi yako ambayo imeharibika.

Pia limao ina kiwango kingi cha vitamin C kinachosaidia seli za ngozi yako kuzalishwa upya na kasi ya ajabu.

Chukua pamba na chovya kwenye juisi ya limao kisha paka sehemu husika kisha acha kwa dk 20 baada ya hapo osha na maji masafi.

Rudia zoezi hili mara 3 hadi 4 kwa wiki moja.
Note: Epuka kutumia juisi ya limao endapo ni muda mfupi umemaliza kunyoa na umejikata sehemu nyeti.

Tango.
Hii pia imekuwa ikishika nafasi kubwa kama ni natural bleaching agent ya ngozi.
Inauwezo mkubwa wa kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kurudisha mpya haraka sana. Na hatimaye kufanya mapaja yako kuwa meupe na sehemu zingine. Chukua kipande cha tango au juisi yake sugua sehemu husika kwa dk 10 hadi 15. Kisha acha angalau dk 10 tena baada ya hapo osha kwa maji ya uvugu vugu.

Pia unaweza kuchukua juisi ya tango,changanya na binzari [unga wake uliosaga] na limao kisha fanya hivyo hivyo. Fanya zoezi hili mara mbili kwa siku.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL