USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Thursday, October 25, 2018

Zitambue mbinu za mafanikio katika kilimo

1. Zalisha kwa wingi.
Uzalishaji mkubwa husaidia sana kupunguza gharama ambazo haziepukiki yani (Fixed Cost). Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo utaweza pia uza bidhaa zako kwa bei ndogo na bado utapata faida nzuri na kujihakikishia soko la uhakika kwa bidhaa zako.

2. Tafuta masoko ya bidhaa kabla ya kuanza uzalishaji.
Mkulima mwenye mafanikio ni lazima pia awe mfanya biashara mzuri ukiachilia mbali kuwa mzalishaji mzuri. Mkulima ni vyema kutengeneza channels mapema kupata wateja wa mazao yako. Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo itakusaidia sana kwenye kupata masoko utakwa na ushawishi zaidi kwa wateja. Tengeneza wateja na wateja watakutengenezea biashara.

Mteja anataka vitu vitatu vya msingi.

  • Unafuu wa bei
  • Ubora wa zao
  • Upatikanaji wa uhakika wa bidhaa

Ukijihakikishia hivyo vitu vitatu hapo juu hapana shaka utakuwa umejihakikishia soko la uhakika

3. Usilime kwa kuafata misimu.
Unapolima kwa kufuata msimu, mtajikuta wakulima wengi mmezalisha zao fulani kwa wiiingi kwa kipindi kimoja hivyo kupelekea upatikanaji wa zao hilo kuwa mkubwa kuliko inavyo hitajika kwenye masoko, jambo hili hupelekea mazao kuuzwa kwa bei ndogo na kupelekea wakulima kukosa faida ya kutosha au hata kupata hasara muda mwingine.

Unapolima kwa kutofata msimu mkulima utaweza kuazalisha zao/mazao kipindi ambacho wengine hawazalishi hivyo mahitaji yatakuwa makubwa na upatikanaji wa zao hilo utakuwa ni mdogo hivyo mkulima ataweza kupanga bei nzuri kwa mazao yake.


4. Epuka kufanya kilimo kwa mazoea

  • Tumia wataalamu wa kilimo
  • Tumia njia za kisasa za kilimo
  • Fanya utafiti wa ardhi dhidi ya zao unalotaka kufanya (Tumia wataalamu)
  • Fanya kilimo cha umwagiliaji uweze kuzalisha kipindi ambacho wengine hawawezi kuzalisha ili uuze mazao yako kwa bei nzuri zaidi
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL