Mbunge wa zamani wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu.
Kumekuwa na madai makubwa ya kununuliwa kwa wabunge nchini kutoka vyama vya upinzani kuelekea chama tawala ambapo madai hayo yanayotolewa na mara kwa mara hasa kwa viongozi na CHADEMA na CUF.
Akizungumza na www.eatv.tv lazaro Nyalandu amesema “wanaohama vyama vya upinzani sijui kama wananunuliwa na sina jibu la hilo, mimi naamini kwamba kwenye demokrasia ya kweli kila mtu ana maamuzi yake na wale wamefanya maamuzi yao, mwisho wa yote kila mtu asimame kwenye sera anazoziamini, na siwezi kuwahukumu wamenunuliwa au hawajanunuliwa.”
Aidha Mbunge huyo wa zamani wa Singida Kaskazini amesema “natamani kuona vyama vya siasa nchini vinavumiliana, na kuondoa uadui baina ya CCM na CHADEMA, pia tujue wote tunataka Tanzania itakayofanikiwa ni fursa ya kutanua wigo wa demokrasia kwa kushindana kwa hoja na sera.”
Mpaka sasa takribani wabunge nane kutoka vyama vya Upinzani wametangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM na kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli licha ya madai ya viongozi wa vyama vyao vya upinzani kudai kuwa wananunuliwa.
0 comments:
Post a Comment