Harmorapa ameeleza kuwa labda haikupangwa kwa yeye kuwa na Wema Sepetu ndio maana hadi sasa hajafanikiwa kuwa naye, hivyo amenyoosha mikono juu kuhusu hilo.
Kilipelekea hilo ni kutokana na Wema Sepetu kuweka wazi kuwa yupo mbioni kuolewa kitu ambacho Harmorapa ameeleza kuwa kimemuumiza sana.
Utakumbuka kuwa kwenye uzinduzi wa movie mpya ya Wema Sepetu, D.A.D uliofanyika Mlimani City wiki kadhaa zilizopita Harmorapa aliibuka na kumkabisha Wema zawadi ya ua kama ishara ya upendo wake kwake.
0 comments:
Post a Comment