USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Thursday, October 25, 2018

Rais Shein apongeza juhudi zinazofanywa na Umoja wa Mataifa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amepongeza juhudi zinazochukuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) katika kuendeleza miradi mbali mbali ya maendeleo na kueleza kuwa kuanzishwa kwa “Program ya Pamoja ya Zanzibar” (ZIP) itakuwa ni kichocheo cha mafanikio.

Rais Dk. Shein ameyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Mratibu mpya wa Umoja wa Mataifa (UN) kwa eneo la Zanzibar Dorothy Temu-Usiri.

Dk. Shein alieleza kuwa kutokana na uzoefu mkubwa wa utendaji kazi wa Mratibu huyo ana matumaini makubwa kuwa program hiyo sio tu itasaidia kuimarisha maendeleo ya Zanzibar bali itasaidia sana katika kufikia malengo ya maendeleo yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa (UN) hapa nchini.

Rais Dk. Shein alisema kwamba, malengo ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa Zanzibar yako wazi katika kila sekta na yanafahamika kwa wananchi wote wa Zanzibar jinsi yalivyolenga katika kuimarisha sekta za maendeleo.

Alisema kuwa (UN) imekuwa ikifanya kazi na kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbalimbali  ikiwemo elimu, afya, upatikanaji wa maji safi na salama, utawala bora, uimarishaji wa haki za binaadamu, uwezeshaji, mapambano ya udhalilishaji wa kijinsia pamoja na uhifadhi wa mazingira.

Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) kwa mashirikiano inayotoa katika kuimarisha miradi mbali mbali ya maendeleo hapa Zanzibar hasa katika masuala ya wanawake na watoto.
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL