Thursday, October 25, 2018
Home »
» Watu watano wafariki katika ajali ya gari la Dangote
Watu watano wafariki katika ajali ya gari la Dangote
WATU watano wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya basi dogo aina ya Haice lenye namba za usajili T760 CUZ kugongwa na lori mali ya kampuni ya Dangote katika eneo la Likahakwa, kijiji cha Mnimbila, mkoani Lindi.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi, kamishna msaidizi wa polisi (ACP) Pudensia Protas na katibu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Lindi (Sokoine),Boniface Lyimo wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake katika manispaa ya Lindi, aliitaja sababu ya ajili hiyo kuwa ni lori la kampuni ya Dangote lenye namba za usajili T973 lenye tela namba za usajili T 515 DAK kuacha mwelekeo wake nakuigonga Haice hiyo iliyokuwa na jumla ya watu sita.
Kamanda Protas alisema kati ya wanawake watatu waliofariki ni pamoja na muuguzi wa zahanati ya Mtumbukile, Salvina Nnunduma. Ambàpo kati ya wanaume wawili waliofariki mmoja ni kondakta wa Basi hilo dogo lililokuwa linafanya safari zake kutoka Kiranjeranje wilaya ya Kilwa kwenda Lindi,Hamis Selemani.
Kamanda huyo alisema aliyesalimika kwenye ajali hiyo aliyoiita ni mbaya miongoni mwa ajali za barabarani zilizowahi kutokea katika siku za hivi karibuni ni dereva wa Basi hilo,anayetambulika kwa jina la Issa Fadhili Makwangu.
" Dereva wa lori alitoweka na kwenda kusikojulikana baada ya kutokea ajali hiyo ambayo imetokea leo asubuhi majira ya saa 1.45.Jeshi la polisi linaendelea kumsaka dereva huyo,"alisema kamanda Protas.
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();







0 comments:
Post a Comment