Msanii wa Bongo Fleva, Rayvanny amejitolea kumsaidia dada ambaye video yake imekuwa ikisambaa kwenye mitandao hivi karibuni ikionyesha akiwa na uvimbe mkubwa jichoni.
Meneja kutokea WCB, Babu Tale ndiye ameeleza kuwa Rayvanny ameonyesha nia ya kumsaidia dada huyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;
"Nimeagizwa na kijana wangu Rayvanny kwa yeyote anayejua huyu dada anapatikana vipi naomba atusaidie ili aweze kumsaidia kutoa msaada kwa kile kidogo alichonacho ila tutaakikisha mpaka atakua salama," ameeleza Babu Tale.
Kwa yeyote anayemfahamu anaweza kuwasiliana na Babu Tale kupitia simu namba +255677011134.
Kwa taarifa tulizonazo huyo dada anaitwa Tumaini Ngamilo kutokea Tukuyu, Mbeya. Anasumbuliwa na tatizo ambalo bado halijajulikana ni nini hasa na lilianza kama uvimbe mdogo lakini hatimaye jicho lote limeharibika na kidonda kinazidi kukua siku hadi siku.
TAZAMA VIDEO YAKE
0 comments:
Post a Comment