Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt Detlef Waechter amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanikiwa kupambana na rushwa nchini na kupata mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi.
Balozi Waechter ameyasem hayo alipofanya mahojiano na Idara ya Habari MAELEZO katika hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Akielezea jinsi rushwa ilivyoota mizizi sehemu nyingi ikiwemo Ujerumani amesema “Tatizo la rushwa sio la Tanzania peke yake, hata pale Ujerumani lipo japo si kwa kiasi kikubwa, bali kila mara serikali inapaswa kujiangalia na kuhakikisha inapambana na mfumo wa rushwa mahala popote. Ili raia wawe na imani na serikali yako”
Kwa dhati kabisa nampongeza Rais Magufuli kwani hali ilikuwa sio nzuri kulingana na ripoti tuliyoisikia wakati wa Mkutano wa 38 wa Bara la Afrika wa Kuthibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya miezi mawili iliyopita. Uwepo wa rushwa Tanzania ilikuwa ni eneo linalotumiwa katika kupitisha madawa hayo ambapo sasa suala hili limepungua kwa kiasi kikubwa kutokanana juhudi za Rais Magufuli," amesema Balozi huyo.
Akielezea ubaya wa rushwa Balozi Waechter amesema kuwa matatizo ya rushwa yanarejesha nyuma maendeleo kwa kuwa watu hawapati huduma wanazostahili kwa kuwa tu kuna wengine wanatumia rushwa. Halikadhalika uwepo wa rushwa unaondoa uaminifu kutoka Taifa moja kwenda linguine au nchi moja kwenda nyingine.
0 comments:
Post a Comment