USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Tuesday, October 23, 2018

C Mwanri aja na mpya nyingine, ajifananisha na Kipa wa Nigeria


Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ameingia kwenye 'headline' tena leo baada ya kusema uwezo wake katika kusakata kabumbu unafanana na Gwiji la Soka nchini, Othman Mambosasa.

Mwanri ametoa kauli yake hiyo katika moja ya ziara zake mkoani humo ambazo zimelenga kushughulikia kero za wananchi wake ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kushughulia changamoto zinazokabili sekta ya michezo.

" Michezo hapa ndio nyumbani kwangu, watu wakiniangalia wanadhani labda sijui utaona safari hii, mimi nacheza nilikua napiga chenga hadi naukalia mpira wenyewe, nilikua nakaa kwenye goli nafanana na Emmanuel Okala au Mambosasa, yaani nikitokelezea namna hii hunifungi halafu kufunga nafunga kama Gattuso nafunga na mguu wa kushoto," amesema Mwanri.

Kwa wale wasiomfahamu Okala huyu alikua Golikipa maarufu wa Timu ya Taifa ya Nigeria na klabu ya Enugu Rangers huku Mambosasa akitamba na Simba SC na Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.

RC Mwanri kwa siku za hivi karibuni amekua akiteka vyombo vya habari na haswa mitandao ya kijamii kutokana na kauli zake ikiwemo misemo yake ya 'Fyekelea mbali, na Sukuma Ndani'
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL