Umoja wa Afrika watoa tamko kuhusu kifo cha Jamal Khashoggi katika tangazo lake lililotolewa Jumanne na muakilishi wake Kwesi Quartey. Katika tamko hilo imetajwa kuwa kifo cha Khashoggi ni jambo la kukemewa.
Katibu msaidizi wa Umoja wa Afrika Kwesi Quartey amefahamisha hayo katika mkutano ulioandaliwa na balozi wa Azerbaijan na kuhudhuriwa na wanadiplomasia.
Mwanahabari huyo wa jarida la Washington Post alipotea tangu Oktoba 2 baada ya kuonekana kwa mara ya mwşsho akiingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul.
Baada ya uchunguzi ulioendeshwa na jeshi la Polisi la Uturuki, Saudia ilikiri kuwa mwanahabari huyo aliuawa katika ubalozi wake ikiwa zaidi ya siku 15 ikidai kuwa aliondoka katika ubalozi huo.
Hadi sasa muili wa Khashoggi haujulikani ulipo. Siku ya kifo cha Khasho watu 15 kutoka Saudia waliwasili mjini Istanbul na kuondoka siku hiyo hiyo.
Wednesday, October 24, 2018
Home »
» Umoja wa Afrika watoa tamko kuhusu kifo cha Jamal Khashoggi
Umoja wa Afrika watoa tamko kuhusu kifo cha Jamal Khashoggi
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment