USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Wednesday, October 24, 2018

Ushirikiano wa Tanzania, Ubelgiji wazidi kukua, Makampuni 41 kutua nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Damas Ndumbaro ametangaza ujio wa makampuni makubwa 41 ya uwekezaji kutoka nchini Ubelgiji ambayo yamepata mwaliko wa Wizara.

Akiongea leo na wanahabari jijini Dar es salaam, Dk Ndumbaro amesema makampuni hayo yatakuwepo nchini kwa siku 4 hadi 5 kwa lengo la kufungua fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo Utalii na Nishati.

"Ushirikiano wetu na Ubelgiji umekuwa mkubwa sasa na kupitia Ubalozi wetu nchini humo umewezesha ujio huu ambapo leo mchana tunawapokea rasmi wageni hao na tuna imani utafungua ajira mbalimbali zikiwemo za moja kwa moja," amesema Dk Ndumbaro.

Amebainisha kuwa wageni hao wataingia leo na kuondoka Oktoba 28 ambapo mbali na shughuli mbalimbali watashiriki katika kongamano kubwa la wafanyabiashara katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambapo tayari wafanyabiashara zaidi ya 200 wa hapa nyumbani wamethibitisha kushiriki.
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL