Home »
HABARI
» Baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari kukanusha kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM, Diwani wa Chadema kata ya Mehenge, Morogoro Mendrad Chipeta ameamua kujiuzulu nafasi zake na kukihama chama hicho. Katika barua yake aliyoandika kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ulanga, Chipeta amesema ameamua kujiuzulu uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM ili aweze kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dk John Magufuli. " Nimetafakari na kuona nikiwa katika chama cha CHADEMA napata wakati mgumu sana wa kuwatumikia wananchi, hivyo nimeona ni busara kwangu kujivua uanachama huo na kuomba kujiunga na CCM ili niungane nao kuwatumikia watanzania chini ya uongozi wa Rais wetu mpendwa Dk John Pombe Joseph Magufuli," amesema Diwani huyo.
Baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari kukanusha kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM, Diwani wa Chadema kata ya Mehenge, Morogoro Mendrad Chipeta ameamua kujiuzulu nafasi zake na kukihama chama hicho.
Katika barua yake aliyoandika kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ulanga, Chipeta amesema ameamua kujiuzulu uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM ili aweze kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dk John Magufuli.
" Nimetafakari na kuona nikiwa katika chama cha CHADEMA napata wakati mgumu sana wa kuwatumikia wananchi, hivyo nimeona ni busara kwangu kujivua uanachama huo na kuomba kujiunga na CCM ili niungane nao kuwatumikia watanzania chini ya uongozi wa Rais wetu mpendwa Dk John Pombe Joseph Magufuli," amesema Diwani huyo.
0 comments:
Post a Comment