Wasanii wawili Mwana FA na Richie wateuliwa kuwa wajumbe wa bodi ya baraza la sanaa taifa (BASATA)
Wasanii wawili wa sanaa mmoja akiwa ni mwanamuziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Hamisi M.Mwinjuma kwa jina maarufu la kazi Mwana FA pamoja na msanii wa Bongo Movie Single Mtambalike alimaarufu Richie wameweza kuwa miongoni mwa wajumbe watano walioteuliwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harison Mwakyembe.
Kufuatia uteuzi uliofanywa na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli wa kumteua bwana Habbi Gunze kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na leo Waziri mwenye dhamana ameweza kuteua wajumbe watano,miongoni mwa wajumbe hao wapo wasanii wawili ambao ni Mwana FA pamoja na Single Mtambulike – Richie.
0 comments:
Post a Comment