Huu ni wimbo wa pili kwa Young Killer kuwashirikisha wasanii hao, wimbo wa kwanza kufanya pamoja unaokwenda kwa jina la 13 ambao ulitoka mwaka 2015.
Hata vivyo katika video ya wimbo huo wa kwanza ambayo iliongozwa na director Nisher Belle 9 hakutokea kwenye video hiyo kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa pande zote mbili.
Awali kabisa Young Killer alimshirikisha Belle 9 kwenye wimbo uitwao Dear Gambe ambao ndio ulimtoa kimuziki. Wimbo huo uliotoka mwaka 2013 ulifanya vizuri hadi kupelekea Young Killer kushinda tuzo ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) kama msanii bora anayechipukia.
SIKILIZA
0 comments:
Post a Comment