USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Tuesday, October 23, 2018

Gekul aikacha Chadema ajiunga na CCM

Aliyekuwa Mbunge Wa Jimbo La Babati Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo [CHADEMA] Paulina Gekul Amepokelewa Rasmi Na Chama Cha Mapinduzi Pamoja Na Aliyekuwa Diwani Wa Kata Ya Maisaka Kupitia Chama hicho Abrahamani Kololi,Mara Baada Ya Kujivua Uanachama Huo kwa kile Walichokieleza ni kuchoshwa na Mambo yanayofanywa na  Chadema.

Akizungumza Na Wananchi  Na Wanachama Wa Ccm Paulina Gekul Alieleza Kuwa Kama Mbunge  Ambaye Yupo  Kwa Ajili Ya Kuwatumikia Wananchi Amefikiri Ni Muda Muafaka Wa Kukiri Ukweli Hadharani Yale Mazuri Ambayo Yanafanywa Na Rais Wetu Lakini Pia Yale Mazuri Yalikuwa Yakifanywa Na Chama Cha Mapinduzi Chama Ambacho Ndio Kina Dola Na Ndio Kina serikali.

“Ni Mengi Mazuri Yamefanywa Katika Jimbo Letu Na Serikali Kuu Haya Mambo Ndio Yaliyonifariji Na Kuonakuwa Kwanini Nisiwe Pamoja Na Hawa Watu Ambao Nikiwa Nao Hapo Nakuwa Na Mh.Rais Na Viongozi Na Wanachama Wa Ccm Ili Kuwaletea Wananchi Maendeleo Na Zile Ndoto Ambazo Mh.Rais Akiwaza Kwa Ajili Ya Watanzania”alisema Gekul
“Sababu Ya Kujiuzulu Ni Kwamba Yale Aliokuwa Akiyapigania Kwaajili Ya Wananchi  Machache Yake Yalikuwa Yakikubalika  Na Yale Ambayo  Na Mengine Kuachwa   Hivyo Ili Kuweza  Kutimizia Wanachi Yale  Aliyowaahidi  Ni Wakati Wa Kuungana Na Viongozi Wa Ccm Kwa Ajili Ya Babati Ambapo Yatakuwa Mepesi Kuliko Vile Ambavyo Walikuwa Wakitofautiana.”

‘’ Kwa Mzigo nilionao Kwa ajili Ya Wananchi Wa Babati niliona mimi Nisiwe Sababu Ya kuwakosesha Haki yenu Kwa Sababu Nipo Upinzani Naamini baada ya Jitihada hizi na Mapokezi Haya Makubwa Babati Yetu Itakuwa Mpya tena,itasonga mbele,na Babati Yetu itasonga mbele na kubadilika kwa sababu tutakuwa tunaongea lugha moja hakuna atayaweza kuzuia’’alisema Gekul.

Kwa upande wake katibu wa siasa na mahusiano ya kimataifa  Kanali Mstaafu Ngemera Lubinga,alisema kwa sasa tayari wamepata watu wa kulinda usalama wa chama na kuzijua njia za adui yao kwa kuwa wale wote wanaotoka upinzani wanazijua njia wanazotumia kwa ajili ya kuharibu mipango ya Ccm.
‘’Niwapongeze wale wote waliorudi Ccm kwani wamerudi wakati ambao tanzania inasema ccm mpya na Ccm mpya hivyo ni wakati wa kutekeleza  majukumu kwa pamoja kwani huwezi kutengeneza jamii mpya kama huna nidhamu ya hali ya juu’’alisema Lubinga.

 Aidha aliwataka wote waliujiunga  na ccm waendane sawa na hitaji la nchi ambalo ni kuwaongoza wananchi kulingana na ilani ya chama cha mapinduzi ikiwa ni pamoja na kuzingatia usiri wa dhamana  ya  uongozi ndani ya  chama ,hivyo basi kwa  kuwa Paulina anataarifa nyingi za adui ni wakati wake wa kupewa majukumu ili aweze  kwenda kupambana na maadui kwa kuwa yeye ndio anajua madaraja ya adui.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti alikipongeza chama cha Mapinduzi  kwa kukubali kuwapokea wanachama wenye akili huku akieleza kuwa unaweza kuwa na chama kikubwa lakini wanachama ni mzigo hivyo kwa kuwa gekul  tayari tupo nae ni matumaini yetu tutafikia tuliyokuwa tunaitaka.

‘’Kuna Taarifa  Kuwa Kuna Watu Wanataka Kujiunga Na Chama Cha Mapinduzi Lakini Tufike Mahali Tuseme Inatosha Kwani Kuna Wanaotaka Kujiunga Na Chama Hiki Kwa Ajili Ya Kutaka Kukivuvunga Na Kuna Taarifa Ambazo Zipo  Kuwa Wanasema Tutawafuata Hukohuko Kuwavuruga Ndio Mana Mi Nasema Tuishie Hapa Hapa Inatosha Kwasababu Tayari Tumeshalamba Madume Magarasha Yabaki Huko Huko Yatatuvuruga Ndo Maana Nasema Inatosha Tumechukua Madume’’alisema Mnyeti.

Naye Mbunge Wa Jimbo La Babati Vijijini Kupitia Chama Cha Mapinduzi Jitu Son Alimpongeza Mbunge huyo Kwa Kujiunga  Ccm Huku akieleza kuwa awali walikuwa wakikutana kwa siri na kufanya mawasiliano kwa siri  kwa ajili ya kujadili masuala ya maendeleo kwa kuhofia lakini kwa sasa itakuwa ni hadharani kwa kuwa lengo ni moja na chama ni kimoja.
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL