USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Thursday, November 15, 2018

Hii ni kwa wapenzi, wachumba au wanandoa, nibora usiwe hewani kuliko kutopokea simu!

Kila mtu anajua maisha ya sasa kuhusu mawasiliano ni simu za mikononi. Simu hizi zimekuwa mwiba katika baadhi ya uhusiano kutokana na baadhi yao kuzitumia kwa usaliti lakini kwa wengine maisha yanaendelea.
Nilikaa nikatafakari malalamiko niliyowahi kuyasikia siku za nyuma na hata karibuni, kwamba baadhi ya wapenzi wameingia kwenye mgogoro kuhusu simu kufuatia kupigiwa na wenza wao halafu hawapatikani hewani au hawapokei tu!

MSINGI WA MANENO NI USALITI

Tabia hii, kila mwenye simu amewahi kukumbana nayo na pengine imewahi kuvunja ndoa kabisa. Wengi wanaamini wenza wao kutopokea simu kunatokana na kuwepo pengine gesti au sehemu nyingine tete kwa hiyo simu ameweka mbali kwa sababu anabanjuka.
Wengine wanaamini ni dharau! Kwamba, mwenza wake anaiona simu ikiita lakini hataki tu kupokea kwa sababu zake binafsi! Hii pia imekuwa ikisababisha ugomvi kwa wapendanao.

UKWELI NI UPI?

Nilipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wasomaji wangu kuhusu hili ambapo baadhi walisema ni afadhali simu ya mwenza wake iite kwa muda mrefu bila kupokelewa kuliko isiwe hewani!
Mimi binafsi kwangu, nikimpigia mume wangu afadhali simu yake iite tu hata mara kumi lakini nisimkose hewani. Ninapomkosa hewani mume wangu nahisi yuko gesti na mwanamke mwingine,” alisema mama Lizi, mkazi wa Makumbusho, Dar.
Mimi tofauti na huyo. Mimi pia afadhali simu iite asipokee kuliko kutokuwa hewani, ila sasa asipokuwa hewani siwazi yuko gesti, bali nawaza amekumbwa na janga zito, pengine hata kifo,” anasema baba Frank, naye mkazi wa Makumbusho.
Mama Mudy, anaishi Kimara-Korogwe, Dar. Yeye anasema: “Mimi mume wangu akitaka tugombane simu yake iite asipokee. Afadhali nipige nigundue haipo hewani kwani anaweza kunidanganya ilizima yenyewe maana si unajua simu zetu za Kichina hizi.
Kusema kweli mimi nikimpigia simu mke wangu halafu ikawa haipatikani hewani nakuwa na amani kuliko asipokee. Maana najua anaiangalia tu na anajua anayepiga ni mimi, nakuwa naumia sana,” anasema Ibrahimu, mkazi wa Buguruni-Kisiwani, Dar.

TABIA INACHANGIA

Nilichobaini ni kwamba, ugomvi wa kutopokea simu wakati inapatikana hewani unatokana na tabia ya mmiliki wa simu. Baadhi ya watu wanajulikana kuwa, hakai mbali na simu yake hata kwa dakika mbili, sasa ikitokea mwenza wake anapiga hapokei anajua anafanya makusudi kwa vile inaaminika hawezi kuwa mbali na simu kwa muda mrefu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL