Mwanzo 4:7
Maandiko haya yanadhihirisha ni kiasi gani ambavyo Mungu wetu anatamani sana sisi
tuweze kuishi maisha ya kumpendeza yeye Mungu wetu.Kuishi maisha matakatifu ya kumpendeza Mungu,yanatupa kibali kwenye maisha yetu ya kila siku kwani mkono wa Mungu wenye nguvu unakuwa pamoja nasi katika kila kitu ukituongoza.Ikiwa tutaishi maisha ya kumpendeza na tukapata kibali kwake tutafanikiwa katika kila jambo ambalo tutalifanya.
TAMBUA KUWA: Kama utaishi maisha matakatifu,basi utakuwa unaongoza na NGUVU ILIYOPO KATIKA UFALME WA MUNGU BABA.
KWA NINI NASEMA SHETANI ANAKUTAMANI UTENDE DHAMBI?
Mwanzo 4:7 imefafanua vizuri kabisa kuwa tusipotenda vyema dhambi iko,inakuotea mlangoni,nayo inakutamani wewe,walakini yapasa uishinde.Maisha ambayo tunaishi,tumezungukwa na mambo mengi sana yenye mvuto wa mtu kumpelekea kufanya maovu/dhambi,kadiri unavyoishi bila kuwa na hofu ya Mungu,ndivyo dhambi inazidi kukuzogelea karibu zaidi na kujikuta umemtenda dhambi Mungu wako.Shetani hutamani zaidi tuanguke katika dhambi/tutende dhambi siku zote,hivyo ufanya kila awezalo ili kutuweka katika mazingira ya kumtenda dhambi Mungu.Acha nikupe mfano huu; kabla sijaokoka,kuna mabinti nilitamani sana kuwapata na kuwa nao kimapenzi,tena ni warembo kweli,kipindi hicho walikataa kuwa nami kabisa,walinitesa sana kimawazo ingawa wapo waliokubali wengi na kuwa nao kimapenzi ila walikuwepo watoto warembo sana ambao wanitesa namna ya kuwapata kwa kipindi hicho,baada ya kuokoka na kuyaacha maisha ya nyuma,ajabu wale mabinti walinitafuta wakinitaka kimapenzi!Pia hata kwa wakati huu nilionao wa neema ya wokovu,nakutana mazingira ya kutongozwa na wadada warembo sana,kwa akili ya kawaida kuwaacha hivi hivi ni ngumu,kinachonipa kushinda ni Kristo yupo ndani yangu na pia kila siku najiweka mazingira ya kutaka kuongozwa na yeye na si akili yangu au dunia hii kama inavyokwenda.
Ukweli ni kwamba,huwezi kushinda mazingira ya kumtenda Mungu dhambi kama huna nguvu ya ulimwengu wa nuru ya Kristo Yesu.
MAMBO YATAKAYOKUFANYA WEWE USHINDE
MAZINGIRA YA
DHAMBI/KUKIKUTA UMEMTENDA MUNGU DHAMBI
1.KUWA MSOMAJI WA NENO LA MUNGU
Ukimpa Mungu nafasi katika maisha yako,ukawa na muda wa kusoma Neno,kujifunza,kuhudhuria kanisani kujifunza Neno la Mungu,utakuwa na mazingira mazuri ya kushinda dhambi kwa sababu pia uwepo wa Roho Mtakatifu utakuwa nawe ukikuongoza katika hatua zako na wewe mazingira ya uovu utayachukia kabisa.NENO LA KRISTO LIKIWA KWA WINGI NDANI YAKO NA UKALIISHI,UTAKUWA MSHINDI.
2.CHAGUA RAFIKI AMBAE HAWEZI KUKUANGUSHA KIIMANI
Rafiki anaweza akawa ni chanzo au mtego wa kukupeleka kwenye uovu na kujikuta unamwacha YESU,na kuingia katika njia ya upotevu wa kumtenda Mungu dhambi.Hivyo kama ni dada uwe na marafiki walio simama kiimani na wenye hofu ya Mungu,na hata kaka pia.Kuwa na marafiki ambao wanawaza wanaume wa kuwachuna au kuuza miili yao,hawa wana weza kukupelekea imani kuacha kwan watakuwa wamekutengenezea mazingira ya wewe kuitamani dhambi na kujikuta umeingikutenda dhambi.
NB; ITAENDELEA
REV; EMMANUEL PAUL SWEYA
0763 53 89 42
Thursday, November 1, 2018
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment