Hivyo kila wakati Muombe mwenyezi ukupe mwanamke mwenye sifa hizi.
Mcha Mungu
Mwanamke mcha Mungu bila shaka maisha yake huwa ya kufanikiwa. Mtu yeyote yule lazima awe mcha Mungu ili awe na sifa nzuri ya maisha katika jamii. Mwanamke mcha mungu huwa na woga na hofu ya mwenyezi Mungu, pia mara nyingi anaogopa katika suala la kutenda dhambi.
Mwaminifu
Hii ni kuanzia kuongea ukweli bila kudanganya hadi maswala ya chumbani. Iwapo mwanamke ana mchepuko mahali fulani ama anamwendea kinyume mpenzi wake, basi aina hii ya tabia haifai kabisa. Sifa ya mwanamke mzuri ni ile ambayo ni ya uaminifu. Mwanamke mwaminifu kwa mpenzi wake haitofika wakati fulani ambapo atakosana na mpenziwe.
Heshima
Heshima haimaanishi ni kwa mpenzi wako pekee bali kwa jamii nzima. Mwanamke ambaye anapenda kugombana na majirani kila kukicha halafu ikifika jioni anamheshimu mpenzi wake hafai. Tabia za mwanamke mzuri ni yule ambaye anaheshimu na kuishi na majirani zake vizuri bila kuwa na mivutano yeyote ile.
Anajiamini
Mwanamke mzuri ni yule anajiamini na anaamini mahusiano yake. Mwanamke mzuri ni yule ambaye hatasikia maneno ya watu halafu akampakizia mpenzi wake. Iwapo kuna suala tata ambalo linafanyika, basi mwanamke aina hii atamwekea kikao mpenzi wake na kujaribu kumuuliza maswali na kutaka kufafanua chochote ambacho kitakuwa kinamkwaza.
Mwanamke aina hii hupendwa na wanaume kwa sababu anajua ya kuwa akifanya jambo fulani basi mpenzi wake atataka kuelezewa bila kuwa na hisia zozote mbaya.
Hivyo Mpenzi msomaji wa Muungwana Blog pindi Utakapokuwa umepata msichana wa mwenye tabia hizo unatakiwa kutangaza ndoa kabisa.
0 comments:
Post a Comment